Posts

BUSH PARTY KUFANYIKA SIKU YA PASAKA KATIKA UFUKWE WA BWALO LA POLISI MWISENGE

Image
Hawa ndio The The Track Masters DJs na Hii ilikua ni siku ya mwaka mpya tulipoangusha bonge la burudani pale bwalo la polisi mwisenge na sasa The track Masters Djs wakishirikiana na Mimi Entertainments & Promotions  tumekuandalia BUSH PARTY ni katika ufukwe wa bwalo la polisi mwisenge kutakua na burudani mbalimbali za toka kwa wasanii wa asili na wasanii mbalimbali wa shows za sebene. Kama kawaida Bonge la Disco kutoka kwa The Track Masters Djs hapa namzungumzia Dj Lima pamoja na Dj Chibarland tutafanya yetu na ww karibu ufanye yako. Burudani itaanza saa nane kamili mchana mpaka choka mwenyewe KINGILIO- Watoto 1000/= na WAKUBWA 2000/= Nyote mnakaribishwa. Imedhaminiwa na AURIC AIR, COCA COLA na POLISI MESS Bwalo la Polisi mwisenge ndio Wadhamini wakuu wa show yetu ya BUSH PARTY siku ya pasaka kumbuka vinywaji vinapatikana kwa bei poa kabisa ya 1500 kwa vinywaji vya TBL karibuni sana kwa burudani na huduma ya vinywaji karibu na bureeeeee ukikosa hii shauri yako Wadhami...

MISS MARA 2013 SASA KUFANYIKA MWANZONI MWA MWEZI WA SITA

Image
Mkurugenzi wa Homeland Entertainments & Promotion Bwana Godsos Mkama( Kulia) Akisisitiza kuwa Mwaka Huu lazima Mkoa wa Mara Utachukua Taji la Miss Tanzania Bila Ubishi. Mkurugenzi wa kampuni ya Homeland Entertainments & Promotions ya Mjimi Musoma Bwana Godsos Mkama amesema shindano la Miss Mara kwa mwaka huu litafanyika wiki ya kwanza ya mwezi wa sita. Akiongea na Chibasa Media House amesema kwa mwaka huu shindano hilo litafanyika baada ya kuwapata wawakilishi kutoka wilaya zote za mkoa wa mara ili kuingia kambini rasmi. Amesema kuwa kwa mwaka huu amejipanga vilivyo kwa udhamini wa kampuni ya bia ya TBL atahakikisha washiriki wake wanafanya vyema kuanzia ngazi ya kanda hadi taifa. Mkama ameongeza kuwa kwa mwaka huu shindano hilo litapambwa na wasanii wakali wa mziki wa kizazi kipya toka dar es salaam na musoma na wasanii hao wako kwenye hatua za mwisho za mazungumzo ili wasaini mkataba. Endelea kutembelea mtandao huu ili uweze kufahamu maandalizi ya shindano hilo la...

MVUVI ANUSURIKA KULIWA NA MAMBA WILAYANI BUNDA

Image
Mamba MVUVI, Yohana Stephano (26), mkazi wa Kijiji cha Guta wilayani Bunda mkoani Mara jana amenusurika kuliwa na mamba wakati akienda kuvua samaki maeneo ya Ziwa Victoria. Akizungumza mara baada ya kufikishwa Kituo cha Polisi Bunda kwa ajili ya kupewa barua ya matibabu, alisema mkasa huo ulitokea majira ya saa moja asubuhi wakati akienda kuvua samaki. Alisema siku hiyo ya tukio aliondoka asubuhi na kuchukua nyavu zake na kwenda ziwani na alipofika ziwani alikwenda sehemu ambako amekuwa akivua samaki kwa kutumia uvuvi wa miguu. “Wakati nikiwa natandaza nyavu yangu ghafla nilishtukia nakamatwa na mamba katika mguu wa kushoto na ndipo nilipokamata majani aina ya matete huku nikipiga kelele za kuomba msaada kwa wavuvi wenzangu ambao pia walikuwa wakijiandaa kwenda kuvua samaki ziwani,”alisema. Alifafanua kuwa baada ya mapambano yake na mamba huyo huku akipiga kelele wananchi na wavuvi wenzake waliwahi kufika kwa kutumia mitumbwi na ndipo walipofanikiwa k...

PROFESA SILAS RWAKABAMBA WA TANZANIA ATEULIWA KUWA WAZIRI WA MIUNDOMBINU RWANDA

Image
Rais wa Rwanda Paul Kagame RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita. Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya. Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi na Menejimenti ya Maafa) na Oda Gasinzigwa (Ofisi ya Waziri Mkuu- Familia na Jinsia). Akizungumza kwa simu na mwandishi wetu jana, mdogo wa Profesa Rwakabamba, Timothy Rwamushaija anayeishi Dar es Salaam, alisema ndugu yake alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Alisema Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na wote baba yao ni Mzee Titus Rwamush...

RAIS MUGABE ATIMIZA MIAKA 89 ASEMA JUKUMU LA KUIONGOZA NI AMRI YA MWENYEZI MUNGU

Image
MUGABE Wafuasi wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe wamekusanyika katika mji wa Bindura wenye migodi ili kusherehekea rasmi Bwana Mugabe kutimiza miaka 89. Ripoti zinasema sherehe hiyo inagharimu dola 600,000 kutokana na mchango wa makampuni. Wenye maduka mjini Bindura wanasema waliamrishwa kufunga maduka mapema hapo jana, ili kusaidia kusafisha mji kwa ajili ya party ya siku ya kuzaliwa ya Bwana Mugabe. Hii ni sherehe ya pili ya Bwana Mugabe kutimiza miaka 89. Katika party ya kwanza iliyofanywa mwezi uliopita Bwana Mugabe alisema jukumu lake la kuongoza Zimbabwe amepewa na Mungu - ni amri ya Mwenyezi Mungu. Wapinzani wake wana wasi-wasi kuwa wafuasi wa Bwana Mugabe wanapanga kuanza tena ghasia na vitisho wakati nchi inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu utaofanywa mwaka huu. Wanasema tayari o...
Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma Wimbi la mauaji limeendelea kushika kasi katika mkoa wa Mara ambapo mnamo tarehe 19/2/2013 katika mtaa wa kawawa kata ya mwigobero manispaa ya Musoma Sabina Dominico aliuwawa kwa kunyongwa kwa kutumia pazia. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma kwa waandishi wa habari binti huyo mwenye miaka 21 alitendewa unyama huo majira ya saa kumi na moja jioni nyumbani kwa magori chacha mfanyabiashara ya mafuta. Taarifa hiyo imeleza kuwa mwili wa marehemu ulikutwa umefungwa mikono na miguu na kisha kamba iliyomnyonga shingoni ni kipande cha pazia alichochanachana. Kabla ya kutekeleza mauaji hayo,Mtuhumiwa huyo ambaye nae alijinyonga kwa kutumia kamba ya manira kwa kujitundika kwenye chuma kinachobeba tanki la maji aina ya simtank na kabla ya kujinyonga alimjeruhi tumboni mke wa mfanyabiashara huyo   Mugesi Magori Chacha   ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa mara kwa ...

LAIBONI MMASAI MWENYE MIAKA 103, WANAWAKE 40, WATOTO 103 NA WAJUKUU KIBAO

Image
ASILIMIA 60 ya watu duniani huamini kuwa hadhi ya mtu kwenye jamii ni kuwa na fedha, magari au nyumba. Hata hivyo , kwa Mzee Meshiko Mapi, Mmasai mwenye umri wa miaka 103, kwake maisha mazuri na yenye hadhi ni wake zake wengi, watoto, wajukuu na ng’ombe wengi wa kutosha. Unapoingia katika eneo lake unamkuta mzee huyu akiwa  katika himaya yake ya kifahari, katika Kijiji cha Esilalee, Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Himaya hiyo ipo katikati ya eneo la Miji midogo ya Makuyuni na Mto wa Mbu.                   Magari yote ya abiria yanayopita  kijijini Esilalee kwenda maeneo mengine, yanakifahamu kituo  maarufu  cha kwa ‘Laiboni.’ Laiboni, ni jina  maarufu la Mzee Mapi na  yeye ndiye mmiliki wa kijiji hicho kwani wakazi wote wa kijiji hicho  ama ni watoto au wajuku zake. Si hivyo tu, bali Shule ya Msingi Laiboni iliyopo katika kijiji hicho nayo ni ...