Posts

ZANZIBAR HEROES YAFUTWA KWA UTOVU WA NIDHAMU KWA KUGAWANA FEDHA BILA UONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA ZANZIBAR

Image
Kikosi cha Timu ya Zanzibar Heroes Kikosi cha timu ya Zanzibar Heroes kimefutwa kwa utovun wa nidhamu, baada ya kushika nafasi ya tatu kikosi hicho katika michuano ya CECAFA, wamegawana fedha bila ya uongozi wa chama cha mpira Zanzibar kufahamu. Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kimechukua uwamuzi wa kuivunja rasmi timu ya taifa, Zanzibar Heroes kufuatia kitendo utovu wa nidhamu kilichofanywa na wachezaji wa timu hiyo,kuamuwa kugawana fedha walizopata baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge yaliyomalizika hivi karibuni mjini Kampala, Uganda. Timu ya Zanzibar heroes ilizawadiwa kiasi cha dola za Kimarekani 10,000 baada ya kuifunga timu ya taifa ya Bara, Kilimanjaro Stars kwa penalti 6-5, baada ya kumalizika mchezo kwa sare ya 1-1. Inadaiwa kuwa wachezaji hao waliamua kugawana fedha hizo kwa madai kuwa wamekuwa wakidhulumiwa f...

TETESI ZIMEENEA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUWA MIKE TYSON ADAIWA KUBADILISHA JINSIA

Image
MIKE TYSON BINGWA wa zamani wa ndondi uzito wa juu, Mike Tyson anadaiwa kubadilisha jinsia kutoka kuwa hali ya kiume na kuwa kike. Habari za kufanyiwa upasuaji huyo kwenye hospitali moja mjini, Beverley Hills, Marekani ziliteka mitandao kadhaa ya kijamii, huku pia gazeti la The Standard likiwa na habari hiyo. Hata hivyo, habari hizo hazijathibitishwa ramsi ingawa mpaka jana jioni mitandano mingi ya kijamii ilikuwa na taarifa hizo. Bingwa huyo wa zamani aliyejitaja kama ëMwanaume mbaya dunianií, mzaliwa wa Brooklyn, aliwaambia waandishi wa habari kuwa siku kwanza atakayopata hedhi (kuona siku zake) ndiyo itakuwa kamilisho la ndoto yake. Lakipi pia katika kuhakikisha anakamilisha dhamira yake ya kuwa mwanamke, amesema kuanzia muda huo jina lake ramsi sasa litakuwa Michelle. Baadhi ya watu wanaweza kudhani mimi ni mtu wa ajabu kwa sababu sasa ni mwanamke," alisema bingwa huyo wa zamani wa ndondi aliyewahu kuhukumiwa kwa shitaka la kubaka. Upasuaji wa kubadi...

NGARIBA HUKO MUGUMU WILAYANI SERENGETI WAMESEMA WATAACHA SHUGHULI HIYO PINDI WAZAZI WATAKAPO ACHA KUWAPELEKA WATOTO KWAO KWA AJILI YA KUKEKETWA

BAADHI ya wanawake wanaoendesha vitendo vya ukeketaji watoto wa kike, maarufu kwa jina la Ngariba, wilayani Serengeti, Mara, wamesema hawawezi kuacha kazi hiyo hadi pale wazazi wenyewe watakapoacha kuwapelekea watoto wao kwa ajili ya kuwakeketa. Akiwawakilisha wenzake juzi, mmoja wa mangariba hao, Agnes Thomas, ambaye ameshiriki kikao cha kupiga vita ukeketaji, kilichoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Mara Inter African Commitee, alisema ni vigumu kuacha kazi hiyo, kwani bado wazazi wengi, wana mwamko wa kuwapelekea watoto wao, ili wakeketwe kwa lengo la kutimiza mila zao. Agnes alisema pamoja na kazi hiyo kuwapatia kipato, lakini ngariba wanaweza kuiacha pale tu wazazi na walezi, watakapobadilika na kuacha tabia ya kuwapelekea watoto. Aidha, wazee wa kimila walioshiriki kwenye kikao hicho, walishauri ili kukomesha ukeketaji; elimu inapaswa kutolewa, ili jamii ifahamu madhara yake. Aidha, katika kikao hicho wazee wa kimila pia walipendekeza itafutwe nj...

MATUMIZI YA LIPSTICK NI HATARI KWA WANAWAKE WAJAWAZITO NA WATOTO

Image
LIPSTICK Wataalamu wa maswala ya afya ya mama na mototo wamewataka wanawake wenye ujauzito kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya Lipstick, imebainika kipodozi hicho kina material yenye madhara kwa afya ya mtoto. Wataalamu hao wamesema kuna umuhimu mkubwa wa kupunguza matumizi ya Lipstick, hasa kwa wanawake wajawazito na watoto wa dogo, mmoja ya wataalamu hao akielezea madhara yaliyopo katika kipodozi hicho pendwa kivutio cha wengi amesema, kila lipstick moja ina Material 55% ya madhara kwa afya ya mtoto. Uchunguzi uliyofanywa na wataalamu hao katika mashirika 22 makubwa duniani yanayojihusisha na utengenezaji wa kipodozi hicho, umebaini kwamba mashirika 12 kati ya 22 yanatumia material yenye madhara kwa watoto, miongoni mwa madhara ya kipodozi hicho, ni kudhofika kwa akili ya motto na kupunguwa uwezo wa kujifunza. Katika siku za hivi karibuni midomo imekuwa sehemu muhimu sana katika ku...

LEMA ATEMA CHECHE KWA WAKAZI WA BUNDA KATIKA MKUTANO WA HADHARA

Image
GODBLESS LEMA AKIWAHUTUBIA WAKAZI WA MJINI BUNDA CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kimemvaa mbunge wa jimbo la Bunda Bw. Stephen Wasira jimboni kwake na kuwataka wakazi wa jimbo hilo kubadili mtazamo wao kwa kuwachagua viongozi wachapa kazi. Akiwahutubia mamia ya wakazi  wa Bunda  juzi katika mkutano wa hadhara mjini Bunda, mjumbe wa mkutano mkuu wa wa taifa CHADEMA Bw. Godbless Lema alisema kuwa matatizo ya watu wa Bunda kamwe hazitaisha kama hawatafanya uamuzi wa kuachana  na Wasira. Alieleza baadhi ya mapungufu ya Wasira ni pamoja na uzee hali inayomsababisha kuzinzia bungeni kutokana na kushindwa kustahimili hoja ngumu zinazoibuliwa na wabunge vijana. “Huyu Wasira kila anapoingia Bungeni ni usingizi tu, katu hawezi kubadilisha Bunda, ni Mzee wa usingizi” alisema Lema a kuongezea. “Watu wa Bunda mlifanya makosa kuwa na mbunge mchapa usingizi bungeni…msisubiri malaika awaondolee usingizi wenu, wapeni CHADEMA nafasi  ili kutafuta uhuru na h...

NELSON MANDELA ALAZWA HOSPITALI KWA AJILI YA KUFANYIWA VIPIMO

Image
NELSON MANDELA ALIYEKUWA Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ametumia usiku katika hospitali katika mji mkuu wa Pretoria. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jana, Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini Jumamosi iliyopita kwa ajili ya kufanyiwa vipimo. Msemaji wa Rais Jacob Zuma, alisema atatoa taarifa zaidi kuhusu hali ya Mandela, baada ya madaktari wake kumaliza kumfanyia vipimo na kutoa taarifa yao ya kitaalamu. Katika taarifa hiyo ya awali, Ofisi ya Rais Zuma ilisema Mandela alikuwa akiendelea vizuri na kwamba kulikuwa “hakuna sababu ya kuwa na mashaka”. Mandela anahitaji matibabu “Mara kwa mara ambayo ni thabiti kutokana na umri wake,” iliongeza taarifa hiyo. Hakuna taarifa kamili juu ya nini kilichosababisha kufikishwa hospitali na haikuwekwa wazi kuwa ni wakati gani Mandela ataruhusiwa kutoka hospitalini. Associated Press liliripoti kuwa wanamaombi walikusanyika katika Kanisa Katoliki la Regina Mundi katika eneo la Soweto huko Johann...

UGONJWA WA MATAMANIO YA KUFANYA MAPENZI MARA KWA MARA WAMSABABISHIA KIFO MWANAMKE MMOJA UFARANSA

Image
Gretchen Molanen Enzi za uhai wake Mwanamke mmoja nchini ufaransa aliyefahamika kwa jina la Gretchen Molanen (23) ameamua kujiua kwa kusumbulia na ugonjwa wa ajabu unaomfanya atamani kufanya mapenzi mara kwa mara bila ya kuishiwa na hamu ya tendo. ungonjwa huo unaofahamika kwa jina Sexxual arousal disorder (female sexual arousal disorde) unazichochea sehemu za siri kutamani kufanya mapenzi mara kwa mara bila ya kuisha hamu. Imelezwa kwamba ugonjwa huo hatari unawapata wanawake tu, kulingana na mtandao mmoja wa kifaransa , unamfanya mwanamke kutamani kufanya ngono wakati wote, bila ya kujali nani anafanya naye tendo hilo, na hakuna kitu kinachoweza kupunguza mataanio hayo mpaka pale hisia hizo zitakapopungua wenyewe, hali hiyo hudumu kwa muda wa masaa kadhaa mpaka siku mzima. Wanasayansi wamesema kwamba ugonjwa huo ni matokeo ya udhaifu na ulegevu wa mishipa ya sehemu za sira za mwanamke, ...