Timu ya wachezaji watumishi wa manispaa ya musoma ipo njia panda kwenda kushiriki katika mashindano ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania Shimisemta

commentsTimu ya wachezaji  watumishi wa manispaa ya musoma huenda ikashindwa kushiriki katika mashindano ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania Shimisemta, baada ya wachezaji wa timu hiyo kudai kuwa hajapewa fedha toka katika ofisi ya mkurugenzi kwa ajili ya kwenda kushiriki katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika huko morogoro.

Wakiongea kwa sharti la kutotajwa majina yao baadhi ya watumishi hao wamesema japokuwa wamekuwa wakitenga muda wao kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo lakini wanashindwa kufanya mazoezi kwa uhakika kutokana na mkurugenzi wa manispaa ya musoma mpaka  kutowathibitishia kwenda kushiriki  katika mashindano huku zikiwa zimebaki siku nne mashindano hayo kuanza.

Wachezaji hao wamedai kuwa wanashindwa kuelewa toka mwaka 2000 timu ya watumishi wa manispaa ya musoma haijashiriki katika mashindano hayo kwa kisingizio cha ufinyu wa bajeti lakini  timu za manispaa ya Musoma vijijini, Bunda, Serengeti pamoja na Tarime zimekuwa zikishiriki katika mashindano hayo kila mwaka.

Jitihada za mwanamichezo wetu kumpata mkurugenzi wa manispaa ya musoma kuzungumzia swala hilo ziligonga ukuta kutokana na kuambiwa yupo nje kikazi.

WANAFUNZI WA MARA SEKONDARI WAANDAMANA WAKIDAI MATIBABU BORA NA CHAKULA BORA

comments
WANAFUNZI WA MARA SEKONDARI WAKIWA KATIKA MAANDAMANO             


Wanafunzi wa shule ya  Sekondari  ya Mara iliyopo  Manispaa ya Musoma mkoani Mara leo wameandamana kuelekea ofisi za mkoa  kile wanachodai kuwa katika shule hiyo hakuna utaratibu  bora wa matibabu na kubadilishiwa  ratiba ya Chakula.

Wakiongea mbele ya Afisa Elimu Mkoa wa Mara Bw Hamis Lisu katika viwanja vya Posta Manispaa ya Musoma, Baadhi ya wanafunzi hao wamesema kuwa kubadilika kwa ratiba ya chakula na kutokuwepo kwa huduma bora za matibabu ndio hali iliyopelekea wao kuandamana ili kufikisha kilio chao katika ngazi ya mkoa.

Wamesema kuwa walipokuwa kidato cha tano ratiba ya kula wali,nyama pamoja na mboga za Majani ilikuwa ni mara mbili kwa wiki lakini tangu January Mwaka huu walielezwa kubadilika kwa ratiba ya chakula kutokana na kugoma kwa mzabuni na hivyo kula wali na nyama mara moja kw wiki  huku mboga za majani hazipatikani kabisa kama wanavyobainisha Alex Mirumbe pamoja na Emmanuel William.

Akiongea mara baada ya kuwasikiliza wanafunzi hao,Afisa elimu Mkoa wa Mara Bw Hamis Lisu aliwaahidi wananfunzi hao kukutana na uongozi wa wilaya na kisha kwenda shuleni hapo ili kutatua madai ya wanafunzi hao.


Mwisho


commentsEmmanuel Chibasa-Mara

Watu wenye ulemavu mkoani Mara wamekutana na uongozi wa mkoa wakiwemo madiwani, wakuu wa idara, pamoja na maafisa maendeleo ya jamii, lengo ikiwa ni kuitambulisha  miongozo ya kitaifa na kimataifa inayoelezea mahitaji na hali halisi ya watu wenye ulemavu ili waweze waweze kuingizwa kwenye mipango kazi pamoja na Bajeti za Halmashauri.

Akiongea katika kikao hicho Abdala Omari ambaye ni mmoja ya wajumbe ya wajumbe wa chama cha walemavu Tanzania SHIVYAWATA ,amesema wameamua kutambulisha miongozo hiyo ili kupunguza changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu kwa kuingizwa kwenye bajeti za Halmashauri hapa nchini ili kuondokana na utegemezi katika jamii.

INSERT: Abdala Omary-Mjumbe Shivyawata

Batista Mgumba ni mwezeshaji kutoka chama cha wasioona Tanzania amesema imefika wakati maswala ya watu wenye ulemavu Tanzania inatakiwa yaingizwe kwenye bajeti za halmashauri wakati wa kupanga mipango pamoja na kupanga bajeti ili waweze kupata huduma sawa kama walivyo watu wengine.

INSERT: Batista Mgumba-Mwezeshaji Chama cha Wasioona Tanzania

Kwa upande wake mwanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ulemavu Elieza Mdakilwa amesema kutokana na watu kutokua na mwamko wa kutetea haki za watu wenye ulemavu hapa mchini ametoa wito kwa taasisi zinazojihusisha na maswala ya watu wenye ulemavu zinatakiwa kuendelea kutetea haki za watu wenye ulemavu kunzia ngazi ya serikali za mitaaa mpaka serikali kuu.

INSERT: Elieza Mdakilwa-Mwanaharakati

Takwimu zinaonyesha kuwa  mkoa wa Mara unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wenye ulemavu hapa nchini kwa kuwa  asilimia 13.
Mwisho

comments


25 Oct 2014

TIMU ya Polisi Mara imeondoka kuelekea mkoani Shinyanga kucheza mchezo wake wanne dhidi ya timu ya Mwadui huku ikitoa tambo ya kufanya mizuri kwenye mchezo huo kutokana na uelewano wa wachezaji.

Akizungumza kabla ya kuondoka kwa timu hiyo yenye maskani yake mjini musoma Afisa Habari wa timu hiyo Musa Keita amesema timu hiyo inaenda kucheza mchezo wa ugenini ikiwa na pointi 7 ikiwa ni ushindi wa michezo miwili na sare moja katika michezo iliyotangulia imewaweka wachezaji katika ari nzuri ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Amesema kwa sasa kikosi cha timu hiyo kipo kwenye maelewano mazuri uwanjani ndio sababu inayowapa Imani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa dhidi ya Mwadui hapo kesho.

Keita alisema wanaondoka kwenda kwenye michezo ya ugenini wakiamini kufanya vizuri kuanzia mchezo huo dhidi ya Mwadui kabla ya kuzifuata timu za JKT Kanembwa na polisi ya Tabora na baadae kurudi nyumbani kwenye michezo mingine.

Akizungumzia michezo mitatu iliyotangulia na kujipatia pointi 7,alisema licha ya timu kufanya vizuri lakini pia wanawashukuru wadau wa soka mkoani Mara kuwapa sapoti kwa kila mchezo na kuomba ushirikiano huo uendelee ili timu hiyo iweze kufanya vizuri kwenye michezo mingine.

Katika michezo iliyotangulia Timu ya polisi Mara ilianza kugawana pointi na timu ya Rhino ya Tabora kwa kufungana bao 1-1 kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya timu ya Green Worrers ya Dar es salaam na Burkinafaso ya Morogoro.


AJALI MBAYA ALIYOIPATA NDUGU YANGU DOMMY MKONO JUMAPILI 10/11/2013 MAGU

comments
BAADA YA AJALI GARI LIKIREKEBISHWA KWA AJILI YA KUVUTWA KULETWA MUSOMA


SEHEMU YA KUSHOTO YA MUONEKANO BAADA YA AJALI
AJALI ILIKUA MBAYA SANA KAMA UNAVYOONA YANI NI KUMUOMBA TU MUNGU SEHEMU YA MBELE YA GARI HILI IMEHARIBIKA VIBAYA
HILI GARI LILILOKUA LIMEPAKI NA KUSABABISHA AJALI  MAENEO YA MAGU
WATU WA USALAMA WAKIPIMA ANGALIA HUO MSTARI UNAONYESHA BREAK ALIZOZOSHIKA DOMI MPAKA ALIPOLIFIKIA ROLI HAPO KWA TRAFIKI WA KIKE.
BAADA YA AJALI KUTOKEA HILI ROLI LILISOGEZWA PEMBENI KABISA YA BARABARA ILI MAGARI MENGINE YAWEZE KUPITA VIZURI
BAADA YA KUMALIZA TARATIBU ZOTE  KATIKA KITUO CHA POLISI MAGU ILIFUATA KAZI YA KULIVUTA GARI HILI KULILETA MJINI MUSOMA NA HII ILIKUA JUMATATU 11/11/2013 SAA 11:16 JION
SEHEMU YA NDANI MBELE PIA ILIHARIBIKA VIBAYA KAMA INAVYOONEKANA BAADA YA AJALI

VIWANGO VYA ALAMA YA MWANAFUNZI NA UFAULU

comments
                                   JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

                                WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI


UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU

UTANGULIZI

Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama CA) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Maoni ya wadau yamekusanywa kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika na utaratibu wake katika mitihani ya kuhitimu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita umekuwa haufanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari. Pia mfumo masuala mbalimbali ya mitihani katika elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa. Kwa sasa kuna miundo mikuu miwili katika mfumo huo.

Muundo wa Kwanza ni upangaji wa viwango katika ngazi ya Shule ambapo Alama Mgando (Fixed Grade Ranges) zifuatazo
hutumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0 – 20. Muundo huu umetumika kwa muda mrefu na umezoeleka kwa walimu na wanafunzi wa elimu ya sekondari kwa ujumla.

Muundo wa Pili ni wa viwango vinavyotumiwa na Baraza la Mitihani la Taifa ambapo ambapo kabla ya mwaka 2012 muundo wa viwango nyumbufu (flexible grade ranges) ulitumika. Katika muundo huu uwigo wa alama ulibadilika badilika kulingana na hali ya matokeo ilivyokuwa kwa mwaka husika. Lakini kuanzia mwaka 2012, Serikali iliamua kutumia mfumo wa Upangaji wa Alama Mgando (Fixed Grade Range) kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumo huu wa alama mgando ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. Kwa upande wa Kidato cha Sita Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E = 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39. Mifumo hii ya Baraza haikuwa inafahamika kwa wadau na hivyo kuwa sehemu ya malalamiko katika sekta ya elimu na mafunzo.

Vilevile, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za CA zitachangia asilimia hamsini (50%) na Mtihani wa mwisho utachangia asilimia hamsini (50%). Kwa upande wa Zanzibar, CA zimekuwa zikiandaliwa kwa mfumo wa asilimia arobaini (40%) na mtihani wa mwisho asilimia sitini (60%). Pamoja na kwamba Baraza halijawahi kuutumia mifumo hii tangu ilipowekwa, kumekuwa na mitazamo, maoni na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya alama za CA. Kuna mawazo pia kwamba mfumo wa CA kuchangia matokeo ya mwisho ya mwanafunzi pia utumike kwa watahiniwa wa kujitegemea (private candidates). Kwa sasa matokeo ya mitihani ya watahiniwa hawa yamekuwa yakitumia alama za mtihani wa mwisho tu na hivyo kutafsiriwa kama utaratibu ambao unamwonea mwanafunzi ambaye anahamu ya kujiendeleza kielimu lakini anakwama kwa sababu mfumo unaotumika siyo rafiki kwa mtahiniwa.

Kwa mantiki hii, Wizara imedhamiria kufanya harmonization ya masuala ya alama katika mitihani ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ili kupata muundo mmoja na ulio wazi kwa wadau wote wa elimu ya sekondari. Lakini pia serikali imedhamiria kuhakikisha tathmini za wanafunzi katika ngazi mbalimbali zinakwenda sambamba na matarajio ya mitaala inayotumika na ambayo inahuishwa mara kwa mara ili iendane na wakati na mahitaji ya elimu katika ngazi mbalimbali.

VIWANGO NA UTARATIBU KUANZIA MWAKA 2013 KWA KIDATO CHA NNE NA KIDATO CHA SITA  KWA MWAKA 2014

Baada ya kufanya tathmini ya maoni mbalimbali ya wadau, misingi ifuatayo ilizingatiwa katika maamuzi kuhusu makundi ya alama na muachano wake:

a)     Alama zitakazotumika zitakuwa A, B, C, D, E na F. Muachano wa alama kati ya kundi moja hadi jingine utafanana, isipokuwa tu pale ambapo itaonekana kuna sababu na hakuna athari za kuwa na muachano tofauti na ule ambao umetumika katika makundi mengine.

b)    Makundi ya alama hayatakuwa na clusters isipokuwa pale ambapo itaonekana kufanya hivyo kunaleta tija katika kupata picha ya wahitimu kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Kwa mantiki hii

(i)      makundi ya alama A, C, D, E na F yabaki na cluster moja moja bali kundi la alama B litakuwa na clusters mbili. Kundi la kwanza litakuwa la wale ambao wamepata alama kati ya 50 mpaka 59 na litaitwa B na lingine litakuwa la wale ambao wamevuka uwigo wa 50 hadi 59 na kuelekea uwigo wa 60 hadi 74 na hili litaitwa B+ (angalia jedwali hapo chini).

(ii)     Pamoja na kuwa na muachano wa alama 26 kama jedwali linavyoonesha hapo chini, alama A kwa miaka mingi imekuwa ikianzia alama 75 hadi 100 na kwamba pamoja na uwigo huo bado wanaofaulu kwa kiwango hicho ni wachache sana. Kwa mantiki hii, hakuna haja ya kubadilisha uwigo ila juhudi ziendelee katika ufundishaji na ujifunzaji ili kiwango cha ufaulu kiongezeke na kupata wanafunzi wengi zaidi wanaofaulu katika kundi hili.

(iii)    Pia, pamoja na kuwa na muachano wa alama 20 kama jedwali linavyoonesha hapo chini kwa miaka mingi, huko shuleni mwanafunzi aliyepata alama 21 na hadi 30 alihesabiwa kuwa na ufaulu wa chini kabisa au hafifu kwa kiwango cha alama D na ingawa ilikubalika ufaulu wa aina hiyo kwa mazingira ya nchi yetu unaridhisha. Alama Filikuwa ni kwa wale waliopata chini ya hapo. Hivyo, alama F itaendelea kuwepo na itaanzia alama 0 hadi 19 na E itaanzia alama 20 hadi 29 na D – 30 -39. Lengo la muundo huu ni kuwa alama mbalimbali, isipokuwa kwa makundi machache, zianzie kwenye 0 yaani 0, 10, 20, 30, 40 na kuendelea badala ya kuanzia kwenye moja yaani 1, 11, 21, 31, 41 na kuendelea. Hii ni kwa ajili ya kuleta mtizamo unaofanana katika ngazi mbalimbali za elimu ambapo kwa sasa ngazi ambazo siyo za elimu msingi na sekondari zinatumia muundo wa kuanzia kwenye 0 badala ya 1.

c)     Uwigo wa jumla wa alama kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita utaendelea kuwa wa alama 0 hadi 100 na kila kundi katika uwigo huu limepewa tafsiri kwa ajili ya kuamua mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya mwanafunzi kulingana na malengo ya mtihani husika. Kimsingi, tafsiri zifuatazo zitakatumika

(i)      Alama A itakuwa na maana ya ufaulu uliojipambanua (distincion or outstanding performance),

(ii)     Alama B+ itakuwa na maana ya ufaulu bora sana (excellent performance),

(iii)    Alama B itakuwa na maana ya ufaulu mzuri sana ( very good perfomance),

(iv)    Alama C itakuwa na maana ya ufaulu mzuri (good performance);

(v)     Alama D itakuwa na maana ya ufaulu wa wastani (low performance),

(vi)     Alama E itakuwa na maana ya ufaulu hafifu (very low performance), na

(vii)   Alama F itakuwa na maana ya ufaulu usioridhisha (unsatisfactory performance).

Wataalamu katika maeneo mbalimbali ya elimu na ulimwengu wa kazi, kwa kushirikiana na Wizara, watatoa maana ya tafsiri hizi kiutendaji katika maeneo yao kulingana pia na mahitaji yao.

d)    Alama C iwe ndiyo alama ya ufaulu mzuri ambao hauhitaji urekebu wa lazima, wakati alama D na E ni alama za ufaulu unaohitaji urekebu kadri mwanafunzi atakavyokuwa anaendelea na masomo ili kuthibitisha kama mlengwa anaweza na kulingana na mahitaji ya eneo husika (targeted remediation). Alama F iwe alama ya eneo linalohitaji urekebu wa hali ya juu (intesive remediation) ili mwanafunzi huyo aweze kumudu masomo kadri anavyoendelea kukua kielimu ama atakapoingia katika ulimwengu wa kazi.

e)     Makundi ya alama yatajumuisha CA kwa kiwango cha asilimia isiyozidi 40 na mtihani wa mwisho kwa asilimia isiyozidi 60 kwa makundi yote ya watahiniwa ikiwemo wale wa kujitegemea (private candidates). Hii ni kwa kuzingatia kwamba CA siyo vizuri izidi uwigo wa alama ya ufaulu mzuri unapoanzia ambayo ni C au 40.

f)      CA kwa upande wa Kidato cha Nne zitokane na mtihani wa Kidato cha Pili (alama 15), matokeo ya Kidato  cha Tatu (alama 5 kwa kila muhula, na hivyo jumla ya alama 10), mtihani wa Mock (alama 10) na kazi mradi  au Projects (alama 5). Kwa upande wa Kidato cha Sita, CA iendelee kutokana na muundo unaotumika sasa.

g)     CA zitumike pia kwa watahiniwa wa kujitegemea. Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegmea ambao wanarudia Mitihani, CA zao  zitumike zile zilizotumika kutoa matokeo yake ya mitihani ya awali.  Kwa watahiniwa wa kujitegemea waliopitia mfumo wa Qualifying Test (QT), matokeo ya QT yatumike kama CA na mtihani wa mwisho uchangie alama 60.

h)    Kwa vile alama endelevu kwa mwaka 2013 kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne tayari zimeshawasilishwa Baraza la Mitihani  Tanzania, alama hizo zichangie asilimia 40 katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2013.

i)       Muundo wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Points Average ama GPA) utaandaliwa na kuanza kutumika pale utakapokuwa tayari na wadau wataelimishwa kuhusu muundo huo ili wapate kuufahamu na manufaa yake katika elimu ya sekondari.

j)       Muundo huu mpya wa alama utatumika kwa mzunguko wa miaka minne kabla haujahuishwa tena ili kuupa muda wa kutosha kuona aina ya changamoto zinazojitokeza na jinsi ya kuzishughulikia. Aina hii ya muda itaruhusu vidato vinne vya elimu ya sekondari ya kawaida na nane ya elimu ya sekondari ya juu kupimwa. Hata hivyo, uhusihaji wa masuala ya mitihani unaweza ukafanyika iwapo matokeo ya uhuishaji wa mitaala kwa ujumla utahitaji pia eneo la mitihani liguswe na kuhuishwa pia.

Kwa mantiki hii, viwango vya alama na ufaulu ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 1 hapa chini:

Jedwali Na 1

MUUNDO WA ALAMA NA UFAULU

ALAMA UWIGO WA ALAMA IDADI YA ALAMA TAFSIRI
A 75 - 100 26 Ufauli Uliojipambanua
B+ 60 - 74 15 Ufaulu bora sana
B 50- 59 10 Ufaulu mzuri sana
C 40 - 49 10 Ufaulu mzuri
D 30 - 39 10 Ufaulu Hafifu
E 20 - 29 10 Ufaulu hafifu sana
F 0 - 19 20 Ufaulu usioridhisha
Kwa aina hii ya muundo wa alama, na kwa kuwa muundo wa GPA utaanza kuandaliwa na wadau kuelimishwa kabla haujaanza kutumika, katika kipindi hiki mpaka wakati huo, muundo wa madaraja utakuwa kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 2 hapa chini.

Jedwali Na 2

MUUNDO WA MADARAJA

MUUNDO WA ZAMANI MUUNDO MPYA MAELEZO
POINTI DARAJA POINTI DARAJA
7-17 1 7-17 I Kundi la ufaulu uliojipambanua na bora sana
18-21 II 18-24 II Kundi la ufaulu mzuri sana
22-25 III 25-31 III Kundi la ufaulu mzuri na wa wastani
26-33 IV 32-47 IV Kundi ufaulu hafifu
34-35 0 48-49 V Kundi la ufaulu usioridhisha
Wataalamu wa mifumo ya mitihani watalifanyia kazi zaidi jedwali hili la madaraja ili liweze kutumika kwa ufanisi katika kipindi hiki cha mpito.

Kwa mantiki hii, Daraja Sifuri linafutwa na kuwekwa daraja litakalojulikana kama Daraja la Tano na ambalo litakuwa ndilo la mwisho kabisa katika ufaulu.

HITIMISHO

Mabadiliko haya yamefanyika ili kuendelea kuimarisha mfumo wetu wa elimu na kuweka wazi taratibu mbalimbali kwa ajili ya mitihani na masuala mengine. Yako mambo mengi mengine ambayo hayana budi kuendelea kuimarishwa ikiwemo mfumo wa mitaala, walimu, mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na vitabu na vifaa vingine muhimu katika elimu. Masuala haya yanaendelea kuangaliwa kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ama Big Results Now (BRN). Ushirikiano wa wadau wote ili kuleta tija kwenye elimu ni muhimu sana na hivyo wizara itaendelea kuwashirikisha wadau wote kwa kadri itakavyohitajika na wadau pia wanaombwa wasiache kuishirikisha wizara pale watakapokuwa na jambo lolote ambalo linahitaji ushirikiano ili kwa pamoja tuweze kupata mafanikio katika sekta ya elimu.Chanzo Wavuti.com

Imetolewa na,

KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI