Timu ya wachezaji watumishi wa manispaa ya musoma ipo njia panda kwenda kushiriki katika mashindano ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania Shimisemta




Timu ya wachezaji  watumishi wa manispaa ya musoma huenda ikashindwa kushiriki katika mashindano ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania Shimisemta, baada ya wachezaji wa timu hiyo kudai kuwa hajapewa fedha toka katika ofisi ya mkurugenzi kwa ajili ya kwenda kushiriki katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika huko morogoro.

Wakiongea kwa sharti la kutotajwa majina yao baadhi ya watumishi hao wamesema japokuwa wamekuwa wakitenga muda wao kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo lakini wanashindwa kufanya mazoezi kwa uhakika kutokana na mkurugenzi wa manispaa ya musoma mpaka  kutowathibitishia kwenda kushiriki  katika mashindano huku zikiwa zimebaki siku nne mashindano hayo kuanza.

Wachezaji hao wamedai kuwa wanashindwa kuelewa toka mwaka 2000 timu ya watumishi wa manispaa ya musoma haijashiriki katika mashindano hayo kwa kisingizio cha ufinyu wa bajeti lakini  timu za manispaa ya Musoma vijijini, Bunda, Serengeti pamoja na Tarime zimekuwa zikishiriki katika mashindano hayo kila mwaka.

Jitihada za mwanamichezo wetu kumpata mkurugenzi wa manispaa ya musoma kuzungumzia swala hilo ziligonga ukuta kutokana na kuambiwa yupo nje kikazi.

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

TOZI GAMBA AFUNIKA SHOW YAKE NA THE TRACK MASTERS DJS BWALO LA POLISI MWISENGE SIKU YA CHRISTMAS