Posts

Showing posts from November, 2014

Timu ya wachezaji watumishi wa manispaa ya musoma ipo njia panda kwenda kushiriki katika mashindano ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania Shimisemta

Timu ya wachezaji   watumishi wa manispaa ya musoma huenda ikashindwa kushiriki katika mashindano ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania Shimisemta, baada ya wachezaji wa timu hiyo kudai kuwa hajapewa fedha toka katika ofisi ya mkurugenzi kwa ajili ya kwenda kushiriki katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika huko morogoro. Wakiongea kwa sharti la kutotajwa majina yao baadhi ya watumishi hao wamesema japokuwa wamekuwa wakitenga muda wao kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo lakini wanashindwa kufanya mazoezi kwa uhakika kutokana na mkurugenzi wa manispaa ya musoma mpaka   kutowathibitishia kwenda kushiriki   katika mashindano huku zikiwa zimebaki siku nne mashindano hayo kuanza. Wachezaji hao wamedai kuwa wanashindwa kuelewa toka mwaka 2000 timu ya watumishi wa manispaa ya musoma haijashiriki katika mashindano hayo kwa kisingizio cha ufinyu wa bajeti lakini   timu za manispaa ya Musoma vijijini, Bunda, Serengeti pamoja na Tarime zim

WANAFUNZI WA MARA SEKONDARI WAANDAMANA WAKIDAI MATIBABU BORA NA CHAKULA BORA

Image
WANAFUNZI WA MARA SEKONDARI WAKIWA KATIKA MAANDAMANO                           Wanafunzi wa shule ya  Sekondari  ya Mara iliyopo  Manispaa ya Musoma mkoani Mara leo wameandamana kuelekea ofisi za mkoa   kile wanachodai kuwa katika shule hiyo hakuna utaratibu  bora wa matibabu na kubadilishiwa   ratiba ya Chakula. Wakiongea mbele ya Afisa Elimu Mkoa wa Mara Bw Hamis Lisu katika viwanja vya Posta Manispaa ya Musoma, Baadhi ya wanafunzi hao wamesema kuwa kubadilika kwa ratiba ya chakula na kutokuwepo kwa huduma bora za matibabu ndio hali iliyopelekea wao kuandamana ili kufikisha kilio chao katika ngazi ya mkoa. Wamesema kuwa walipokuwa kidato cha tano ratiba ya kula wali,nyama pamoja na mboga za Majani ilikuwa ni mara mbili kwa wiki lakini tangu January Mwaka huu walielezwa kubadilika kwa ratiba ya chakula kutokana na kugoma kwa mzabuni na hivyo kula wali na nyama mara moja kw wiki  huku mboga za majani hazipatikani kabisa kama wanavyobainisha Alex Mirumbe pamoja na E