Posts

Showing posts from 2013

AJALI MBAYA ALIYOIPATA NDUGU YANGU DOMMY MKONO JUMAPILI 10/11/2013 MAGU

Image
BAADA YA AJALI GARI LIKIREKEBISHWA KWA AJILI YA KUVUTWA KULETWA MUSOMA SEHEMU YA KUSHOTO YA MUONEKANO BAADA YA AJALI AJALI ILIKUA MBAYA SANA KAMA UNAVYOONA YANI NI KUMUOMBA TU MUNGU SEHEMU YA MBELE YA GARI HILI IMEHARIBIKA VIBAYA HILI GARI LILILOKUA LIMEPAKI NA KUSABABISHA AJALI  MAENEO YA MAGU WATU WA USALAMA WAKIPIMA ANGALIA HUO MSTARI UNAONYESHA BREAK ALIZOZOSHIKA DOMI MPAKA ALIPOLIFIKIA ROLI HAPO KWA TRAFIKI WA KIKE. BAADA YA AJALI KUTOKEA HILI ROLI LILISOGEZWA PEMBENI KABISA YA BARABARA ILI MAGARI MENGINE YAWEZE KUPITA VIZURI BAADA YA KUMALIZA TARATIBU ZOTE  KATIKA KITUO CHA POLISI MAGU ILIFUATA KAZI YA KULIVUTA GARI HILI KULILETA MJINI MUSOMA NA HII ILIKUA JUMATATU 11/11/2013 SAA 11:16 JION SEHEMU YA NDANI MBELE PIA ILIHARIBIKA VIBAYA KAMA INAVYOONEKANA BAADA YA AJALI

VIWANGO VYA ALAMA YA MWANAFUNZI NA UFAULU

                                   JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA                                 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU UTANGULIZI Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama  CA ) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Maoni ya wadau yamekusanywa kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika na utaratibu wake katika mitihani ya kuhitimu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita umekuwa haufanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari. Pia mfumo masuala mbalimbali ya mitihani katika elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa. Kwa sasa kuna miundo m

KABURI LA MTOTO ALIYEFARIKI MIAKA MITATU ILIYOPITA LAFUKULIWA BAADA YA KUONEKANA YUKO HAI

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida kaburi ambalo alizikwa mtoto Shabani Maulidi (15), ambaye anadaiwa kufariki dunia miaka mitatu iliyopita na kuonekana akiwa hai hivi karibuni, jana lilifukuliwa na viungo vya mwili wake kukutwa ndani. Kazi hiyo iliyofanyika chini ya ulinzi mkali wa polisi pamoja na Mtafiti wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mwanza, Lucas Ndungulu, ilizua taharuki kwa umati wa watu waliokuwa eneo hilo, baada ya nyumba ya jirani lilipo kaburi hilo, Masanja Marwa, kubomoka ghafla wakati ufukuaji huo ukiendelea, huku mwanamke mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja naye akianguka na kuzirai. Kwa sasa mtoto huyo ambaye alionekana hai, amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa uangalizi wa kitaalamu. Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, Ndungulu alisema kuwa wameamua kufukua kaburi hilo ili kupata sehemu ya viungo vya mwili kwa ajili ya vipimo. “Lengo la kufukua kaburi hili ni kutaka tupate kiungo chochote cha

WATAKAO FELI MTIHANI WA KIDATO CHA PILI KURUDIA DARASA

Image
Wanafunzi Wakati wanafunzi wa kidato cha pili wakitarajia kufanya mtihani wa taifa wiki ijayo, Serikali imesema watakao feli watarudia darasa hilo. Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi profesa Sifuni Mchome alipokua akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam. Alisema jumla ya wanafunzi 531, 457 wa kidato cha pili wanatarajia kufanya mtihani huo nchi nzima. “ watakao feli watarudia darasa hilo na watakao feli mara ya pili serikali itaangalia uwezekano wa kuwapeleka shule za ufundi au kuendelea na shule kama wanafunzi wa kujitegemea” alisema Profesa sifuni. Alisema mtihani huo utaanza October 7 hadi 21 mwaka huu katika vituo takribani 4,437 vilivyosajiliwa kwa ajili ya kufanyia mitihani nchi nzima na wanafunzi waliojiandikisha kufanya mitihani hiyo wasichana ni 270,734 sawa na asilimia 50.1 na wavulana ni 260,723 sawa na asilimia 49.1 ambao ni sawa na ongezeko la asilimia 3.1 ikilinganishwa na watahiniwa wa mwaka jana

JESHI LA POLISI NCHINI LIMEMFUKUZA KAZI ASKARI ALIYEINGIA UKUMBI WA DISCO AKIWA NA BUNDUKI

KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu na majambazi, maarufu kama Kimbunga, Simon Sirro, amesema kuwa wamemtimua askari wao aliyeingia ukumbi wa disko mjini Bukoba akiwa na bunduki kwa ajili ya kulipa kisasi. Sirro alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jana wakati akielezea mafanikio waliyoyapata katika operesheni hiyo kwa kuwakamata watuhumiwa 88 wanaojihusisha na ujambazi na biashara ya silaha. Alimtaja askari huyo kuwa ni mwenye namba H 85, PC Alphonce, aliyekuwa ametokea mkoani Mara kwa ajili ya kushiriki operesheni hiyo mkoani Kagera. Alisema kuwa PC Alphonce alikorofishana na baadhi ya watu ndani ya ukumbi wa disko, hivyo akatoka nje kufuata bunduki, kisha akarudi nayo kwa ajili ya kuwadhuru ‘wabaya’ wake, lakini askari wenzake waliokuwamo ndani walifanikiwa kumzuia kabla ya kutimiza azima yake. Kuhusu kukamatwa kwa Mkurugenzi wa redio ya kijamii iliyoko wilayani Karagwe (FADECCO) na kuwekwa ndani siku mbili, kis

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA AFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MARA KUBORESHA MAHUSIANO

Wito umetolewa kwa wanasiasa na wanachama wa chama cha mapinduzi Mkoani Mara kuacha Siasa za makundi ndani ya chama ili kukimalisha na kuboresha utendaji kazi wa chama hicho. Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) Mkoani Mara Bwana Christopher Mwita Sanya, alipokua akijibu maswali mbalimbali toka kwa Waandishi wa Habari Mkoani Mara katika ofisi za chama hicho zilizopo mtaa wa nyasho mjini Musoma. Sanya amesema siasa za makundi hazitakiwi kwani zinarudisha nyuma maendeleo ya chama na Taifa kwa ujumla na tayari chama hicho kimeanza vikao vyenye lengo la kuondoa makundi na kuboresha utendaji kazi wa chama hicho. Amesema chama hicho kimejiwekea utaratibu wa kuwakumbusha madiwani na wabunge wa chama hicho kutekeleza ahadi wanazotoa kwa wananchi ili kurejesha imani kwa wananchi kuwa ahadi wanazotoa katika chaguzi mbalimbali wanazitekeleza. Mwenyekiti huyo wa chama cha mapinduzi mkoani mara leo amefanya kikao hicho na waandishi wa habari kwa len

MUDA WA KUBADILISHA LESENI SASA MWISHO APRIL 31

Matatizo ya kukatika kwa umeme ni miongoni mwa sababu zilizosababisha polisi nchini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulazimika kuongeza muda wa utoaji wa leseni mpya hadi Aprili 31 mwaka huu badala ya Machi 31 iliyopangwa. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alisema wamelazimika kuongeza siku baada ya kubaini kuwapo kwa mambo kadhaa yaliyokwaza baadhi ya madereva kubadilisha leseni zao kama inavyotakiwa. “Tumebaini madereva hao walishindwa kubadili leseni zao kutokana na kukosekana kwa mtandao ambao ndiyo unawezesha mawasiliano ya kielektroniki kati ya TRA na trafiki, ingawa pia siku za kazi ziliingiliana na Sikukuu ya Pasaka’’ alisema. Alisema baadhi ya madereva wengine nao  hawajamaliza mafunzo yao ya PSV katika Vyuo vya NIT na Veta huku wengine wakichelewa kupewa vyeti vyao licha ya kumaliza mafunzo hayo,”alisema Mpinga. Alisema kutokana na sababu hizo wameamua kuongeza muda ikiwa ni mw

SERIKALI KUCHUKUA HATUA KALI KWA WATAKAOTUMIA VIBAYA SIMU NA MITANDAO YA KIJAMII

SERIKALI imesema itachukua hatua kali za kisheria kwa atakayebainika kutumia vibaya simu za mkononi, na mitandao ya kijamii kuleta uchochezi au kwenda kinyume na maadili ya nchi. Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alipozungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka kukomesha vitendo hivyo. “Hatua hizo zitachukuliwa dhidi ya kampuni au mtu yeyote atakayetoa kashfa na kuitukana serikali, viongozi wa serikali, dini, siasa na watu binafsi,” alisema na kuongeza kuwa vitendo hivyo vinakiuka sheria za nchi. Alisema hatua hizo pia zitawakumba watu wote wanaojihusisha na uonyeshaji wa picha za ngono kwenye mitandao, unyanyasaji wa watoto na ukiukaji wa maadili na kutoa taarifa zenye lengo la kuvunja utulivu na amani. “Matumizi mabaya ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kama simu za mikononi, barua pepe, na mitan

BUSH PARTY KUFANYIKA SIKU YA PASAKA KATIKA UFUKWE WA BWALO LA POLISI MWISENGE

Image
Hawa ndio The The Track Masters DJs na Hii ilikua ni siku ya mwaka mpya tulipoangusha bonge la burudani pale bwalo la polisi mwisenge na sasa The track Masters Djs wakishirikiana na Mimi Entertainments & Promotions  tumekuandalia BUSH PARTY ni katika ufukwe wa bwalo la polisi mwisenge kutakua na burudani mbalimbali za toka kwa wasanii wa asili na wasanii mbalimbali wa shows za sebene. Kama kawaida Bonge la Disco kutoka kwa The Track Masters Djs hapa namzungumzia Dj Lima pamoja na Dj Chibarland tutafanya yetu na ww karibu ufanye yako. Burudani itaanza saa nane kamili mchana mpaka choka mwenyewe KINGILIO- Watoto 1000/= na WAKUBWA 2000/= Nyote mnakaribishwa. Imedhaminiwa na AURIC AIR, COCA COLA na POLISI MESS Bwalo la Polisi mwisenge ndio Wadhamini wakuu wa show yetu ya BUSH PARTY siku ya pasaka kumbuka vinywaji vinapatikana kwa bei poa kabisa ya 1500 kwa vinywaji vya TBL karibuni sana kwa burudani na huduma ya vinywaji karibu na bureeeeee ukikosa hii shauri yako Wadhamini w

MISS MARA 2013 SASA KUFANYIKA MWANZONI MWA MWEZI WA SITA

Image
Mkurugenzi wa Homeland Entertainments & Promotion Bwana Godsos Mkama( Kulia) Akisisitiza kuwa Mwaka Huu lazima Mkoa wa Mara Utachukua Taji la Miss Tanzania Bila Ubishi. Mkurugenzi wa kampuni ya Homeland Entertainments & Promotions ya Mjimi Musoma Bwana Godsos Mkama amesema shindano la Miss Mara kwa mwaka huu litafanyika wiki ya kwanza ya mwezi wa sita. Akiongea na Chibasa Media House amesema kwa mwaka huu shindano hilo litafanyika baada ya kuwapata wawakilishi kutoka wilaya zote za mkoa wa mara ili kuingia kambini rasmi. Amesema kuwa kwa mwaka huu amejipanga vilivyo kwa udhamini wa kampuni ya bia ya TBL atahakikisha washiriki wake wanafanya vyema kuanzia ngazi ya kanda hadi taifa. Mkama ameongeza kuwa kwa mwaka huu shindano hilo litapambwa na wasanii wakali wa mziki wa kizazi kipya toka dar es salaam na musoma na wasanii hao wako kwenye hatua za mwisho za mazungumzo ili wasaini mkataba. Endelea kutembelea mtandao huu ili uweze kufahamu maandalizi ya shindano hilo la

MVUVI ANUSURIKA KULIWA NA MAMBA WILAYANI BUNDA

Image
Mamba MVUVI, Yohana Stephano (26), mkazi wa Kijiji cha Guta wilayani Bunda mkoani Mara jana amenusurika kuliwa na mamba wakati akienda kuvua samaki maeneo ya Ziwa Victoria. Akizungumza mara baada ya kufikishwa Kituo cha Polisi Bunda kwa ajili ya kupewa barua ya matibabu, alisema mkasa huo ulitokea majira ya saa moja asubuhi wakati akienda kuvua samaki. Alisema siku hiyo ya tukio aliondoka asubuhi na kuchukua nyavu zake na kwenda ziwani na alipofika ziwani alikwenda sehemu ambako amekuwa akivua samaki kwa kutumia uvuvi wa miguu. “Wakati nikiwa natandaza nyavu yangu ghafla nilishtukia nakamatwa na mamba katika mguu wa kushoto na ndipo nilipokamata majani aina ya matete huku nikipiga kelele za kuomba msaada kwa wavuvi wenzangu ambao pia walikuwa wakijiandaa kwenda kuvua samaki ziwani,”alisema. Alifafanua kuwa baada ya mapambano yake na mamba huyo huku akipiga kelele wananchi na wavuvi wenzake waliwahi kufika kwa kutumia mitumbwi na ndipo walipofanikiwa k

PROFESA SILAS RWAKABAMBA WA TANZANIA ATEULIWA KUWA WAZIRI WA MIUNDOMBINU RWANDA

Image
Rais wa Rwanda Paul Kagame RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita. Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya. Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi na Menejimenti ya Maafa) na Oda Gasinzigwa (Ofisi ya Waziri Mkuu- Familia na Jinsia). Akizungumza kwa simu na mwandishi wetu jana, mdogo wa Profesa Rwakabamba, Timothy Rwamushaija anayeishi Dar es Salaam, alisema ndugu yake alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Alisema Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na wote baba yao ni Mzee Titus Rwamush

RAIS MUGABE ATIMIZA MIAKA 89 ASEMA JUKUMU LA KUIONGOZA NI AMRI YA MWENYEZI MUNGU

Image
MUGABE Wafuasi wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe wamekusanyika katika mji wa Bindura wenye migodi ili kusherehekea rasmi Bwana Mugabe kutimiza miaka 89. Ripoti zinasema sherehe hiyo inagharimu dola 600,000 kutokana na mchango wa makampuni. Wenye maduka mjini Bindura wanasema waliamrishwa kufunga maduka mapema hapo jana, ili kusaidia kusafisha mji kwa ajili ya party ya siku ya kuzaliwa ya Bwana Mugabe. Hii ni sherehe ya pili ya Bwana Mugabe kutimiza miaka 89. Katika party ya kwanza iliyofanywa mwezi uliopita Bwana Mugabe alisema jukumu lake la kuongoza Zimbabwe amepewa na Mungu - ni amri ya Mwenyezi Mungu. Wapinzani wake wana wasi-wasi kuwa wafuasi wa Bwana Mugabe wanapanga kuanza tena ghasia na vitisho wakati nchi inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu utaofanywa mwaka huu. Wanasema tayari o
Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma Wimbi la mauaji limeendelea kushika kasi katika mkoa wa Mara ambapo mnamo tarehe 19/2/2013 katika mtaa wa kawawa kata ya mwigobero manispaa ya Musoma Sabina Dominico aliuwawa kwa kunyongwa kwa kutumia pazia. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma kwa waandishi wa habari binti huyo mwenye miaka 21 alitendewa unyama huo majira ya saa kumi na moja jioni nyumbani kwa magori chacha mfanyabiashara ya mafuta. Taarifa hiyo imeleza kuwa mwili wa marehemu ulikutwa umefungwa mikono na miguu na kisha kamba iliyomnyonga shingoni ni kipande cha pazia alichochanachana. Kabla ya kutekeleza mauaji hayo,Mtuhumiwa huyo ambaye nae alijinyonga kwa kutumia kamba ya manira kwa kujitundika kwenye chuma kinachobeba tanki la maji aina ya simtank na kabla ya kujinyonga alimjeruhi tumboni mke wa mfanyabiashara huyo   Mugesi Magori Chacha   ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa mara kwa matibabu.