Posts

Showing posts from April, 2013

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA AFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MARA KUBORESHA MAHUSIANO

Wito umetolewa kwa wanasiasa na wanachama wa chama cha mapinduzi Mkoani Mara kuacha Siasa za makundi ndani ya chama ili kukimalisha na kuboresha utendaji kazi wa chama hicho. Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) Mkoani Mara Bwana Christopher Mwita Sanya, alipokua akijibu maswali mbalimbali toka kwa Waandishi wa Habari Mkoani Mara katika ofisi za chama hicho zilizopo mtaa wa nyasho mjini Musoma. Sanya amesema siasa za makundi hazitakiwi kwani zinarudisha nyuma maendeleo ya chama na Taifa kwa ujumla na tayari chama hicho kimeanza vikao vyenye lengo la kuondoa makundi na kuboresha utendaji kazi wa chama hicho. Amesema chama hicho kimejiwekea utaratibu wa kuwakumbusha madiwani na wabunge wa chama hicho kutekeleza ahadi wanazotoa kwa wananchi ili kurejesha imani kwa wananchi kuwa ahadi wanazotoa katika chaguzi mbalimbali wanazitekeleza. Mwenyekiti huyo wa chama cha mapinduzi mkoani mara leo amefanya kikao hicho na waandishi wa habari kwa len

MUDA WA KUBADILISHA LESENI SASA MWISHO APRIL 31

Matatizo ya kukatika kwa umeme ni miongoni mwa sababu zilizosababisha polisi nchini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulazimika kuongeza muda wa utoaji wa leseni mpya hadi Aprili 31 mwaka huu badala ya Machi 31 iliyopangwa. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alisema wamelazimika kuongeza siku baada ya kubaini kuwapo kwa mambo kadhaa yaliyokwaza baadhi ya madereva kubadilisha leseni zao kama inavyotakiwa. “Tumebaini madereva hao walishindwa kubadili leseni zao kutokana na kukosekana kwa mtandao ambao ndiyo unawezesha mawasiliano ya kielektroniki kati ya TRA na trafiki, ingawa pia siku za kazi ziliingiliana na Sikukuu ya Pasaka’’ alisema. Alisema baadhi ya madereva wengine nao  hawajamaliza mafunzo yao ya PSV katika Vyuo vya NIT na Veta huku wengine wakichelewa kupewa vyeti vyao licha ya kumaliza mafunzo hayo,”alisema Mpinga. Alisema kutokana na sababu hizo wameamua kuongeza muda ikiwa ni mw

SERIKALI KUCHUKUA HATUA KALI KWA WATAKAOTUMIA VIBAYA SIMU NA MITANDAO YA KIJAMII

SERIKALI imesema itachukua hatua kali za kisheria kwa atakayebainika kutumia vibaya simu za mkononi, na mitandao ya kijamii kuleta uchochezi au kwenda kinyume na maadili ya nchi. Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alipozungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka kukomesha vitendo hivyo. “Hatua hizo zitachukuliwa dhidi ya kampuni au mtu yeyote atakayetoa kashfa na kuitukana serikali, viongozi wa serikali, dini, siasa na watu binafsi,” alisema na kuongeza kuwa vitendo hivyo vinakiuka sheria za nchi. Alisema hatua hizo pia zitawakumba watu wote wanaojihusisha na uonyeshaji wa picha za ngono kwenye mitandao, unyanyasaji wa watoto na ukiukaji wa maadili na kutoa taarifa zenye lengo la kuvunja utulivu na amani. “Matumizi mabaya ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kama simu za mikononi, barua pepe, na mitan