Posts

Showing posts from February, 2013
Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma Wimbi la mauaji limeendelea kushika kasi katika mkoa wa Mara ambapo mnamo tarehe 19/2/2013 katika mtaa wa kawawa kata ya mwigobero manispaa ya Musoma Sabina Dominico aliuwawa kwa kunyongwa kwa kutumia pazia. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma kwa waandishi wa habari binti huyo mwenye miaka 21 alitendewa unyama huo majira ya saa kumi na moja jioni nyumbani kwa magori chacha mfanyabiashara ya mafuta. Taarifa hiyo imeleza kuwa mwili wa marehemu ulikutwa umefungwa mikono na miguu na kisha kamba iliyomnyonga shingoni ni kipande cha pazia alichochanachana. Kabla ya kutekeleza mauaji hayo,Mtuhumiwa huyo ambaye nae alijinyonga kwa kutumia kamba ya manira kwa kujitundika kwenye chuma kinachobeba tanki la maji aina ya simtank na kabla ya kujinyonga alimjeruhi tumboni mke wa mfanyabiashara huyo   Mugesi Magori Chacha   ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa mara kwa matibabu.

LAIBONI MMASAI MWENYE MIAKA 103, WANAWAKE 40, WATOTO 103 NA WAJUKUU KIBAO

Image
ASILIMIA 60 ya watu duniani huamini kuwa hadhi ya mtu kwenye jamii ni kuwa na fedha, magari au nyumba. Hata hivyo , kwa Mzee Meshiko Mapi, Mmasai mwenye umri wa miaka 103, kwake maisha mazuri na yenye hadhi ni wake zake wengi, watoto, wajukuu na ng’ombe wengi wa kutosha. Unapoingia katika eneo lake unamkuta mzee huyu akiwa  katika himaya yake ya kifahari, katika Kijiji cha Esilalee, Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Himaya hiyo ipo katikati ya eneo la Miji midogo ya Makuyuni na Mto wa Mbu.                   Magari yote ya abiria yanayopita  kijijini Esilalee kwenda maeneo mengine, yanakifahamu kituo  maarufu  cha kwa ‘Laiboni.’ Laiboni, ni jina  maarufu la Mzee Mapi na  yeye ndiye mmiliki wa kijiji hicho kwani wakazi wote wa kijiji hicho  ama ni watoto au wajuku zake. Si hivyo tu, bali Shule ya Msingi Laiboni iliyopo katika kijiji hicho nayo ni ya kwake na  baadhi ya wanafunzi  wa shule hiyo ni watoto na hata wajukuu zake.  Kijiji hiki kimepambwa kwa mandhari