Posts

Showing posts from December, 2012

TOZI GAMBA AFUNIKA SHOW YAKE NA THE TRACK MASTERS DJS BWALO LA POLISI MWISENGE SIKU YA CHRISTMAS

Image
ikafika muda tozi na sinyorita wakapiga mavazi kivingine makamuzi ya tozi yanaendelea Hapa nikitoa maelekezo kwa watoto kuondoka make muda wao ulikua umekwisha Hapa ni sehemu ya jikoni na Albert hapa anaweka order ya mchemsho siku ya krismac Wadau wa The Track Master walifika asubuhi kutoa sapoti wakati wa maandalizi kutoka kulia ni mshikaji wetu ALBET wa vodacom akiwa na fans wetu wengine Denis wa muwasa mwenye shati jeupe Viunga tofauti tofauti ambavyo vimedizainiwa kwa ubunifu wa hali ya juu pale bwalo Hii ndio Kaunta ya nje ambayo inatumika kwa sasa Haya ndio mandhari halisi ya ufukwe wa bwalo la polisi yani kumetulia sana ebu fika pale upate huduma safi ya vinywaji na chakula kwa bei poa kabisa Nyomi ilikua ya kutosha katika ufukwe wa bwalo la polisi mwisenge eneo lote lilijaa watu balaaa usichezee The Track Masters Djs weweeeeeeeeeeeeeee Watoto walikuja kwa wingi sana bwalo la polisi hii ni kudhirisha kuwa tozi gamba ndio habari ya mjini haku

KONTENA LA KONDOMU FEKI LAKAMATWA BANDALINI JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Kondomu KONTENA lililosheheni kondomu za kiume kutoka nchini India imekamatwa na kuzuiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kubainika kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu. Maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamelazimika kufanya msako mkali kwenye baadhi ya maduka ya dawa jijini Dar es Salaam baada ya kubainika kwamba tayari kondomu hizo zipo sokoni. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Leandri Kinabo alizitaja kondomu hizo kuwa ni aina ya Melt Me zenye thamani ya Sh222.1   milioni zilizokamatwa tangu Oktoba 23 mwaka huu na kuzuiliwa bandarini hapo kwa taratibu zaidi za kisheria. “Jambo lililotushtua ni kwamba zimebainika kwamba zipo madukani, tukajaribu kufuatilia tena bandarini tukifikiri kuwa huenda zimetolewa kinyemela licha ya kuzuiliwa ili ziteketezwe au zirejeshwe nchini India kwa gharama zao wahusika. Tulipokwenda bandarini tukabaini kwamba bado zipo katika hali ile ile, kumbe  zimein

HOSPITALI YA MKOA WA MARA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA BAADHI YA DAWA

Image
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara Iragi Ngerageza Hospitali ya Mkoa wa Mara inakabiliwa na upungufu wa baadhi ya dawa zinazotolewa na bohari ya dawa (msd) hali inayopelekea dawa zinazokosekana kununuliwa kwenye maduka binafsi yaliyoteuliwa na serikali. Akiongea na chibasa blogspot mganga mfawidhi w badoa hospitali hiyo Iragi Ngerageza amesema kuwa bohari ya dawa imekuwa ikiwapa dawa ambazo hazitoshelezi mahitaji ya hospitali hiyo. Amesema kuwa hivi karibuni hospitali hiyo imenunua dawa kwenye bohari ya dawa zenye thamani ya shilingi 41,190,100 lakini bado kuna mahitaji ya baadhi ya dawa hali inayosababisha wananchi kwenda kununua madawa kwenye maduka ya mitaani. Katika kukabiliana na tatizo hilo tayari uongozi wa hospitali kupitia kamati yake inafanya jitahada ya kununua dawa ambazo hawakuzipata kutoka bohari ya dawa (msd) kwenda kununua dawa hizo kwenye maduka ya watu binafsi ambayo yameteuliwa na serikali. “Wananchi wanatakiwa kuelewa kuwa tunaupu

KIPIMO CHA X-RAY KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA MARA KIMEFANYIWA MATENGENEZO

Image
MGANGA MFAWIDHI WA HOSPITALI YA MKOA WA MARA IRAGI NGERAGEZA AKITOA MAELEZO KWA BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI. BAADHI YA WAANDHI WA HABARI MKOANI MARA WAKIWA NA MGANGA MFAWIDI WA HOSPITALI YA MKOA WA MARA KUTOKA KUSHOTO NI HELLEN MAGABE, IRAGI NGERAGEZA AMBAYE NDIE MGANGA MFAWIDHI, EMMANUEL CHIBASA NA LAZARO KAAJI Baadhi ya wagonjwa wanaokwenda hospitali ya Mkoa wa Mara kupima kipimo cha X-ray wamelalamikia uongozi wa hospitali hiyo kutotoa taarifa kwa wagonjwa baada ya kukosekana kwa huduma hiyo kwa muda. Wakiongea na gazeti hili leo wakiwa nje ya chumba cha x-ray mmoja wa wagonjwa Bi Mage Hilary amesema toka siku ya jumatatu amekuwa akiwahi kila siku asubuhi ili kupata huduma hiyo lakini ameshindwa kuipata na hakuna taarifa yoyote toka kwa daktari kwa nini hataki kuwahudumia. “Ndugu mwandishi hii sio haki kabisa we fikiria toka asubuhi tuko hapa na hakuna taarifa yoyote toka kwa daktari kwanini huduma haitolewi tunawaona tu madaktari wanapita hapa wanatuona k

UTAFITI WA WANASAYANSI WAONYESHA TUNDA LA TIKITI MAJI LINASAIDIA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME

Image
T Watafiti wa nchini Marekani wamegundua kwamba matikiti maji yanaongeza nguvu za kiume na yanasaidia kutoa tiba kwa wanaume wenye upungufu wa nguvu za kiume.     Watafiti katika chuo kikuu cha Texas A&M wamegundua kwamba matikiti maji yanaweza yakatumika kama "Viagra ya Asili" kwa wanaume wenye matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Watafiti hao walisema kuwa tikiti maji lina amino acid nyingi za citrulline ambazo huifanya mishipa ya damu itanuke na iwe katika hali kama ile ambayo mtu anayetumia viagra au madawa ya kuongeza nguvu za kiume huwa nayo. Citrulline ikiwa mwilini hugeuka kuwa "arginine" mojawapo ya aina za amino acid. Hali hii husababisha kuongezeka kwa kiwango cha nitric oxide kwenye damu. Nitric oxide husaidia kuifanya mishipa ya damu itanuke. Hata hivyo watafiti hao hawakuweka wazi idadi ya matikiti maji ambayo mwanaume anatakiwa kula ili aweze kuwa na nguvu za kiume kama za viagra. Bhimu Patil, mkurugenzi wa maabara iliyofa

MBUNGE WA MUSOMA MJINI VICENTI NYERERE ASEMA BULEMBO AMEINGIZWA MJINI

Image
VICENTI NYERERE MBUNGE WA MUSOMA MJINI MBUNGE wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (CHADEMA), amekana kumtambua mtu aliyejinadi alikuwa Meneja wa Kampeni wa jimbo hilo, Juma Songo, ambaye amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema chama hicho kimetapeliwa. Akizungumza na Tanzania Daima juzi, Nyerere alisema aliyekuwa meneja kampeni wake ni Fikiri Malenge, ambaye mpaka sasa ni katibu wake na wala si Songo. Nyerere alisema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa CCM, Abdallah Bulembo, amekutana na watoto wa mjini na kumdanganya, naye akajikuta anadanganyika kama mtoto mdogo. “Bulembo hakujua kama Musoma kuna watoto wa mjini, sasa kaingizwa chaka bovu naye kaingilika kwa kudanganywa kampeni meneja wangu alikuwa huyo Songo wakati kampeni meneja wangu ni Fikiri Malenge,” alisema. Nyerere alisema CCM haikuwa makini katika mambo yake ndiyo maana wakapokea mtu aliyewadanganya, nao wakakubali na kuutangazia umma bila kuhakiki. Alisema tabia ya kukurupuka kwa

MAMA ATAKA KUJIUA KWA KUNYWA SUMU BAADA YA KUFIWA WATOTO WATATU

Image
Mama mmoja Mkoani Mara, amechukuwa uwamuzi wa kunywa sumu baada ya kugunduwa watoto wake watatu wamefariki dunia, watoto hao walikufa kwa kukosa hewa, baada ya kuacha jiko la mkaa lililokuwa limeinjikwa maharage likiwa linawaka na kwenda kulala. Mama huyo alichukua uwamuzi huo mgumu na wahatari wa kunywa sumu baada ya kuamka na kugunduwa kuwa watoto wake watatu wamefariki dunia, mama huyo aliwaishwa hospitali na kufanikiwa kutapishwa sumu aliyokunywa. Watoto hao walikufa kutokana na kukosa hewa katika chumba walichokuwa wamelala ambacho kulikuwa na jiko la mkaa lililokuwa likipika maharage, lna kusababisha kukosa hewa na kupelekea vifo kwa watoto hao. Watoto hao watatu waliyofariki ni wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Nyangoto, iliyopo katika Tarafa ya Ingwe wilayani Tarime Mkoani Mara, Naomi Nyasenso darasa la saba, Magreth Nyasenso darasa la nne na Debora Nyasenso darasa la kwanza. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime, Kamishina Msaidizi Justus Kamugisha, amewashauri wan

HAUKIMIWA KWENDA JELA MIAKA SABA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NOTI BANDIA

Image
PESA ZA TANZANIA MAHAKAMA ya wilaya ya Musoma mkoani Mara, imemhukumu kwenda jela miaka 7 mfanyabiashara  Mayai Justine(28) mkazi wa Nyakato Mshikamano kwa kosa la kupatikana na noti bandia. Akisoma hukumu hiyo   siku ya ijumaa ,mahakamani hapo   , Hakimu mfawidhi mwandamizi wilaya ya Musoma, Richard Maganga baada ya kuridhika na ushahidi  alimhukumu Justine  kutumikia kifungo cha miaka 7. Mbele ya hakimu, Mwendesha mashtaka wa serikali  Jonas Kaijage amedai kuwa Bw. Mayai Justine ambaye ni mkazi wa Nyakato Mshikamano mjini Musoma  alipatikana na noti bandia za shilingi elfu 50 April 13 mwaka huu na kufikishwa mahakamani Mei 17, 2012. akitoa hukumu hiyo Hakimu Maganga amesema kupatikana na noti bandia ni kosa la jinai hivyo ametoa hukumu hiyo hili iwe fundisho kwa wafanyabiashara wanaoweza kufanya kosa kama hilo.

TAFITI ZA KISAYANSI ZINAONYESHA KUWA ULAJI SANA WA NYAMA NYEKUNDU UNASABABISHA UPOFU

Image
ULAJI SANA WA NYAMA NEKUNDU UNASABABISHAUPOFU Watu wanaopenda sana kula nyama nyekundu kama vile nyama za ng'ombe , mbuzi au 'kitimoto' wana uwezekano mkubwa wa kupata upofu kwenye uzee wao.   Matokeo ya utafiti wa wanasayansi umegundua kwamba watu wanaopenda kula sana zaidi ya mara kumi kwa wiki nyama za ng'ombe, mbuzi au kondoo na nguruwe wana uwezekano wa asilimia 50 wa kupata upofu kulinganisha na wale wanaokula nyama hizo chini ya mara tano kwa wiki. Utafiti huo pia umeonyesha kuwa watu wanaopenda sana kula nyama za kuku walionekana kuwa na kinga dhidi ya ugonjwa unaosababisha upofu kutokana na kuharibika kwa retina ya jicho unaojulikana kitaalamu kama Age-related macular degeneration (AMD) ambao husababisha upofu kwa wazee wenye umri zaidi ya miaka 50. Utafiti huo ulifanywa na chuo kikuu cha Melbourne cha nchini Australia ambapo wanaume na wanawake 5,600 wenye umri wa kwenye miaka ya hamsini na sitini walifanyiwa majaribio kwa miaka 13. Ingawa

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) YAWATOA WASIWASI WATANZANIA KUHUSU MFUMO WA DIGITALI

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewatoa hofu wananchi wote wanaoishi katika maeneo ambayo bado kufikiwa na mfumo mpya wa mawasiliano wa digitali, akisema wataendelea kupata mawasiliano kupitia mfumo wao wa zamani wa analojia. Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Meneja wa Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Innocent Mungi wakati akifafanua kuhusu wasiwasi uliojitokeza kwa wananchi hasa walioko mikoani. Mungi alisema watazima mtambo wa zamani kule ambako huduma hiyo mpya ya digitali imefika, kwamba kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na mtambo huo, wataendelea kutumia televisheni zao kupitia mfumo wa zamani. Alibainisha kuwa, hadi sasa ni asilimia 24 sawa na mikoa 11 ya nchi ndiyo itafaidika na mawasiliano hayo ya digitali, ambapo kule kusikokuwa na mawasiliano hayo bado wataendelea kupata mawasiliano kwa kutumia satelaiti, madishi na usambazaji wa nyaya hadi hapo mfumo mpya utakapowafikia. “Naomba niwatoe hofu wananchi kuwa siyo kweli kwamba i

MWALIMU AKUTWA AMELALA UCHI KATIKA KIBAO CHA SHULE HUKO LINDI

Image
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za kishirikina. Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam. Akizungumzia tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma kutokana na kuwa na usingizi mzito.Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha  ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa Kwa upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa, wamekosa molari wa ku

WAKAZI WA INDONESIA WAANZISHA UTAMADUNI WA KUWAFUKUA MAITI NA KUWATEMBEZA MTAANI KABLA YA KUZIKWA TENA

Image
Mmoja ya Maiti ikipambwa kabla ya kufanyiwa Sherehe Wakazi wa Jimbo la Twaraj Indonesia, wamejiweka utamaduni wa kuwafufua maiti(wafu) na kuwapamba kwa kuwavisha mavazi mapya, kuwachana nywele na kuwatembeza mitaani kabla ya kuwazika tena.   Dunia imejaa vituko na matukio ya ajabu, hilo limedhihirika hivi karibuni huko nchini Indonesia, katika jimbo la Twaraj, wakazi wa eneo hilo wanatamaduni ya ajabu na ngeni duniani, wakazi hao wanawafufuwa maiti kaburini na kuwavalisha nguo mapya za thamani, kuwachana nywele na kuwapamba kamalive walivyokua hai. Wakazi hao wanakusanyika na kumfanyia sherehe kubwa maiti kabla ya kuanza msafara wa kumtebeza katika mitaa na kumrejesha kaburini alipokuwa amezikwa, wakazi hao wanamini kwamba watu waliyokufa wanahaki ya kuendelea kuishi na kujumuika nao. katika kufanikisha zoezi hilo la kihistoria ambalo wanaimani kwa lazima kufanya ili kuonesha hishima kwa maiti na kulinda mapenzi ya kweli kwa mtu aliyekufa, kabla ya kumzika maiti

MFANYAKAZI WA KAZI ZA NDANI AMNYWESHA MKOJO BOSI WAKE KWA KUMCHELEWESHEA MSHAHARA

MFANYAKAZI za ndani ‘hausigeli’ amehukumiwa kifungo cha miezi miwili jela na viboko, kwa kosa la kumnywesha mkojo bosi wake kutokana na hasira ya kutolipwa mshahara wake kwa wakati. Rita Chakwesha mwenye umri wa miaka 25, ambaye aliajiriwa katika nyumba iliyopo kwenye Barabara ya Avenue mjini Harare, kwa makusudi alimnywesha mwajiri wake Sharlotte Chivavarirwa maji yaliyokuwa na mkojo ndani yake. Chakwesha alionekana mbele ya Hakimu Barbra Masinire huko Harare, akihukumiwa kwa makosa hayo, huku akijitetea kuwa alikuwa akifanya hivyo kutokana na kutopewa ujira wake kwa miezi miwili. Mshauri wa Jimbo la Francesca Mukumbiri aliiambia mahakama kuwa Novemba 5 majira ya saa 11 jioni, Chivavarirwa alirejea nyumbani akitokea kazini, na mara baada ya kufika alimwomba msichana wake wa kazi Chakwesha ampe maji kutoka katika jokofu. Chakwesha alienda na kumiminia maji ambayo tayari alikuwa ameyatia mkojo na kumpa bosi wake kwamba ayafurahie kwani ni maji yaliyokuwa na ladha

MWANAMKE AKERWA KUPEWA TARAKA KWENYE MTANDAO WA FACEBOOK

Image
Emma na Nail Brady wakati wa Harusi Yao Mwanamke mmoja nchini Uingereza alipigwa na butwaa baada ya kugundua kwamba ndoa yake ya miaka sita imefikia tamati baada ya kugundua kwamba mumewe amemuachia talaka kwenye mtandao wa Facebook. Emma Brady, 39, alisema kwamba aligundua kwamba ameachika baada ya kupigiwa simu na rafiki yake baada ya rafiki yake huyo kuona talaka yake kwenye mtandao wa Facebook. Ujumbe uliorushwa kwenye mtandao huo ulisomeka "Neil Brady ameamua kuvunja ndoa yake na Emma Brady." Bi Brady aliielezea aibu aliyoisikia na hasira kutokana na talaka hiyo iliyowekwa kwenye mtandao na kusomwa na watu kadhaa. Emma aliiambia mahakama ya Blackburn ambayo mume wake mwenye umri wa miaka 39 mtaalamu wa IT alikutwa na hatia ya kumshambulia. "Nilijisikia vibaya sana kutokana na tukio hili. Watu wote ambao ninawasiliana nao kwenye mtandao ni watu ambao nimejuana nao kwa miaka mingi, nilijihisi kuaibishwa sana kwa jambo hili kuwekwa wazi katika mta