Posts

Showing posts from November, 2012

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

Image
Kati ya Kuku na Yai Kipi Kilianza? Mjadala wa miaka mingi kuhusiana na kipi kilitokea mwanzo kuku au yai? umepata jibu baada ya wanasayansi kuthibitisha kuwa kuku ndiye aliyekuwepo awali kabla ya yai. Mjadala wa miaka nenda rudi kuwa kuku na yai kipi kilitangulia duniani umepatiwa jibu na wanasayansi wa nchini Uingereza ambao wamethibitisha kuwa kuku ndiye aliyekuwepo mwanzo kabla ya yai. Kwa kuangalia jinsi ganda la yai lilivyotokea, wanasayansi wa nchini Uingereza wanaamini wamepata jibu la mjadala huo. Watafiti katika vyuo vikuu vya Sheffield na Warwick nchini Uingereza wamegundua kuwa protini inayoitwa ovocleidin (OC-17) ni muhimu sana katika kutengenezwa kwa gamba la yai. Lakini protini hiyo hupatikana toka kwenye ovari ya kuku mwenye ujauzito. Kwa maana hiyo yai lisingekuwepo kama kusingekuwa na protini ambayo inatoka kwa kuku mjamzito. Watafiti hao waliongeza kuwa protini ya OC-17 husababisha calcium carbonate kwenye mwili wa kuku ibadilike kuwa calcite crys

TAHADHARI UKIWEKA LAPTOP MAPAJANI ZINAUA NGUVU ZA KIUME NA KUHARIBU MBEGU ZA KIUME

Image
Scott Reed aliathirika kwa kuweka Laptop Mapajani I Imethibitishwa kitaalamu kuwa joto linalotolewa na laptop inapotumika ikiwa mapajani hupelekea kuharibika kwa mbegu za kiume na kuwafanya wanaume washindwe kupata watoto na wapenzi wao.   Scott Reed alifikiria kwenda na mkewe hospitali kujaribu njia ya kupandikiza mimba baada ya kuhangaika muda mrefu kujaribu kupata mtoto bila mafanikio. Kitu ambacho Scott hakuweza kukifikiria ni pale alipoambiwa na madaktari kuwa laptop yake anayoitumia mara kwa mara akiwa ameiweka mapajani ndio chanzo cha tatizo lake la kutopata mtoto. Madaktari walimuambia kuwa joto linalotokana na laptop yake inapotumika ikiwa mapajani husababisha kuharibika kwa mbegu za kiume na hivyo kumfanya ashindwe kupata mtoto. Scott mwenye umri wa miaka 30 aliamua kuanza kuitumia laptop yake akiwa ameiweka kwenye meza na matunda yake yalijionyesha baada ya miezi mitatu ambapo mkewe Laura ambaye naye ana umri wa miaka 30 alipopata ujauzito. Hivi sasa iki

CHAMA CHA WANAHABARI WANAWAKE (TAMWA) KUTOA MAFUNZO YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA

Image
Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania(TAMWA) Kinatarajia kuendesha mafunzo kwa Waandishi wa habari Mkoani Mara ili waweze kuibua na kuandika habari za Ukatili wa kijinsia. Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho Valerie Msoka mafunzo hayo yanalenga kuadhimisha siku 16 za kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia na lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa Habari  kuripoto swala la ukeketaji na kuandika habari zaidi kuhusu swala hilo. Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa Mkoa wa Mara ndio unaongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ukifuatiwa na mkoa wa dodoma. Waandishi wa habari Mara kupitia chama cha waandishi wa habari mkoa (MRPC) Wanatarajia kushiriki mafunzo hayo kikamilifu ili waweze kuibua na kuripoti habari za ukatili wa kijinsia ili kutokomeza tatizo hilo Chama hicho hapa nchini kinaendesha miradi kadhaa ikiwa ni pamoja na harakati za usawa wa kijinsia na kuhakikisha kuwa wanawake wanashiriki vyema katika kucha

WANASAYANSI UJERUMANI WAGUNDUA DAWA INAYOWEZA KUWAZUA WANAUME KUTEMBEA NJE YA NDOA

Image
FIDELITY HORMON Wana sayansi wana mambo sikia hii huko nchini ujerumani Sasa kumegunduliwa dawa aina ya homoni inayoweza kuwazuia wanaume kwenda nje, au kuwa na uhusiano wa pembeni, Dawa hii iliyovumbuliwa Ujerumani inaitwa FIDELITY HORMON. Dawa ya uaminifu! Au kampuni hiyo ya ujereumani imeipa dawa hiyo jina la CUDDLE DRUG! Dawa ya kukumbatiana. Dr René Hurle­mann, of Bonn University nchini Ujerumani anasema mwanamume akipewa dawa hii ya kumeza huyeyuka na kuingia katika damu, hivyo mwanamke mrembo akipita karibu, basi mume analazimika kukaa umbali wa inchi sita . Mume bila kujua damu yake itakuwa haipatani na mwanamke mwengine mbali na mkewe. Mwanamke huyo akiwa mrembo zaidi , ndio dawa inafanya kazi vizuri zaidi. Ni FIDELITY HORMON. Tembe za uaminifu.Chanzo bbc

AUWAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MISHALE NA KUKATWA MAPANGA WILAYANI TARIME AKIGOMBEA ARDHI

Image
Justus Kamugisha Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Tarime na Rorya Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha ng’ereng’ere   wilayani tarime ameuwawa kikatili kwa kuchomwa mishale na kukatwa katwa kwa mapanga . Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa kanda maalum ya kipolisi ya Rorya na Tarime Kamishina Msaidizi Justus Kamugisha   amesema kuwa tukio hilo limetokea jana   majira ya saa mbili asubuhi   ambapo amemtaja aliyeuwawa kwa kuchomwa mishale na mapanga ni Robert   Chacha   kabila mkurya -mkira   44) mkazi   wa kijiji cha Ng’ereng’ere Kata ya Nyamaraga   Tarafa ya Inchugu wilayani Tarime. Kamugisha amesema kuwa jeshi la polisi linamshikilia juma chacha mwita (22) wa kijiji cha   korotambe   ambaye   amekiri   kufanya hivyo na wenzake saba ambao wamekimbia na polisi wanaendelea kuwatafuta. Chanzo cha mauaji hayo ni marehemu kulima katika   eneo linalogombaniwa   na koo hizo ambapo serikali   ilikataza eneo hilo lisitumike kwa shughuli za kilimo ili kuepusha migogo

SHILINGI MILIONI 800 ZATUMIKA KUNUNUA VIFAA VYA VILABU 23 VYA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA BARA NA ZANZIBAR

Image
Katibu Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Mara Beldina Nyakeke akipokea sehemu yaVifaa Jumla ya shilingi milioni 800 zimetumika kununua vifaa vya vilabu 23 vya waandishi wa habari Tanzania bara na zanzibar vilivyoanza   kutolewa jana   na muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania UTPC kwa lengo la kuwaongezea ufanisi wa kazi zao ambapo mikoa ya Mwanza ,Mara na Kagera imekuwa ya kwanza kukabidhiwa seti   13 ya vifaa hivyo kila mmoja. Hafla   hiyo ya makabidhiano ya   vifaa   vya ofisi   za klabu   za waandishi wa habari   Imefanyika   jana katika ofisi za utpc jijini mwanza mtaa wa isamilo ambapo rais wa utpc keneth simbaya   alikabidhi   vifaa   vyenye thamani ya milioni   105 kwa vilabu vitatu vya mwanza,mara na kagera ambapo kila klabu thamani yake ni milioni 35   na kuwataka viongozi   waliopokea vifaa hivyo   kwenda kuvitumia kwa makini   na si kuhoziwa na viongozi   na badala yake   wapange    mipango mikakati itakayowawezesha kujitegemea kwa kubuni mir

AGUNDUA ANA ALEJI NA MBEGU ZA KIUME ZA MME WAKE SIKU YA HARUSI

Image
Mike na Jullie Boyde Siku ya Harusi Usiku wa furaha ya harusi uligeuka kuwa usiku wa majonzi baada ya wanandoa kugundua kuwa hawataweza kuwa na uwezo wa kupata mtoto katika maisha yao ya ndoa kwa kuwa bi harusi ana aleji na mbegu za kiume za mumewe. Mike mwenye umri wa miaka 27 na Julie Boyde mwenye umri wa miaka 26 wakazi wa Ambridge, Pennsylvania nchini Marekani walikuwa katika mapenzi moto moto kwa miaka miwili kabla ya kuamua kufunga ndoa na kuamua kufanya mapenzi bila kutumia kinga kwa mara ya kwanza usiku wa harusi yao. Lakini mambo hayakuenda vizuri kama walivyotarajia kwani ghafla iligundulika kuwa bi harusi alikuwa na aleji na mbegu za kiume za mumewe. Muda mfupi baada ya Mike kuziachia mbegu zake za kiume, Bi harusi alipatwa na maumivu makali sana ambayo mwenyewe anayaelezea kuwa ni sawa na kama mtu alikuwa akipigilia misumari ndani ya mwili wake. Maumivu hayo yaliyoambatana na vipele yaliendelea kwa wiki kadhaa kabla ya kutoweka. Baada ya vipimo kadhaa

MUSOMA YAPATA MABILIONI TOKA BENKI YA DUNIA KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO MUSOMA MJINI

Image
HALMASHAURI ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara, imepata msaada wa zaidi ya sh bilioni 21 kutoka Benki ya Dunia (WB). Fedha hizo zitaanza kutolewa Julai mwaka 2013 na zitatolewa kwa miaka mitatu ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Musoma mjini. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma, Alex Kisurura, alisema hayo jana mjini hapa alipozungumza na Tanzania Daima kuhusu mipango ya maendeleo kwa wakazi wa mji huo na kujinasibu kwamba katika kipindi cha miaka mitano manispaa hiyo itafurahia mafanikio ya kisekta. Kwa mujibu wa mstahiki huyo fedha hizo za ufadhili wa Benki ya Dunia zimelenga kutekeleza miradi ya kiuchumi ikiwemo miundombinu ambapo kila mwaka benki hiyo itatenga fedha ili kufikia malengo ya maendeleo. “Manispaa ya Musoma tumekubaliwa na Benki ya Dunia kupewa dola milioni 14.1 za Marekani kuanzia Julai 2013 na tutapewa kwa awamu tatu kila mwaka wa fedha! “…Licha ya Benki ya Dunia kutupa fedha hizi imetupa masharti ya kuhakikisha matumizi yak

ALIYE KUWA WAZIRI WA KWANZA WA SHERIA NCHINI UFARANSA RACHIDA DATI ADAI KUWA HAJUI NANI BABA WA MTOTO WAKE KWA KUWA ALIKUA NA MAHUSUANO YA KIMAPENZI NA WANAUME WANANE KWA KIPINDI KIMOJA

Image
Rachida Dati Aliyekuwa waziri wa kwanza mwanamke wa sheria nchini Ufaransa, Rachida Dati amedaiwa kuwa hajui nani ndiye baba wa mtoto wake kwakuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wanane kwa kipindi kimoja. Rashida Dati mwenye umri wa miaka 47 amedaiwa kuwa alikuwa bize kwenye kubadilisha mabwana kiasi cha kwamba hajui ni mwanaume gani ndiye aliyempa mimba. Dati amemfikisha mahakamani bilionea Dominique Desseigne, 68, akidai ndiye baba wa binti yake Zohra kufuatia uhusiano wao wa kimapenzi mnamo mwaka 2008. Desseigne amegoma kupima DNA akisema kuwa yeye alikuwa miongoni mwa wanaume wanane waliokuwa wakitembea na waziri huyo wa zamani wa sheria nchini Ufaransa. Katika ushahidi wa maandishi uliotolewa na wanasheria wa bilionea Desseigne umeweka wazi kuwa Dati alikuwa na mahusiano na wanaume wanane katika kipindi kimoja na imewataja wanaume hao kuwa miongoni mwao yumo aliyekuwa waziri mkuu wa Hispania, Jose Maria Anzar na aliyekuwa rais wa Ufaransa, Sark

MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA MARA YAVUKA LENGO KATIKA UKUSANYAJI KODI TOKA MWEZI JULAI HADI OCTOBA 2012

Image
TANZANIA REVENUE AUTHORIRTY                             Mamlaka ya Mapato ya Mkoa wa Mara imevuka   malengo   kwa kukusanya   kiasi cha shilingi bilioni 23. na kuvuka   lengo lililokusudiwa   la shilingi bilioni 22.2 kwa kipindi cha julai hadi oktoba 2012. Hayo yamesemwa   leo na meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Mara Joseph Kalinga   wakati akitoa taarifa   ya ukusanyaji wa mapato   kwa mgeni rasmi katibu tawala wa Mkoa wa Mara Clement Lujaji . Kalinga amesema kuwa ili kufanikisha utoaji wa huduma   yenye   ubora wa hali ya juu na  ya kuvutia   kwa mlipakodi   , idara ya huduma   na elimu   kwa mlipa kodi ,imekuwa   ikitoa semina mbalimbali zenye lengo la kuwaelimisha   walipa kodi sheria   za kodi ,haki za mlipa kodi,wajibu wa mlipa kodi na wajibu wa mamlaka ya mapato imeongeza ushirikiano   baina ya walipa kodi   na watoza   kodi   pamoja   na kuinua   kiwango cha ulipaji   kodi kwa hiari. Amesema kuwa hali ya makusanyo   kwa mwaka wa fedha wa 2011/12,Mkoa wa

TIMU YA WAANDISHI WA HABARI YAITANDIKA TRA MARA 2-1 KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI KUELEKEA KUADHIMISHA SIKU YA MLIPA KODI

Image
Benchi la ufundi likifuatilia kwa umakini kambumbu kutoka kushoto ni Emmanuel Almas, George Marato, Shomari Binda,Thomas Dominick na Emmanuel Chibasa Wachezaji wa Timu ya waandishi wa habari wakisherekea ushindi mara baada ya mpira kumalizika kati yao kuanzia Kulia ni Denis Magoti,dj Cares One,Dj Lima wakionyesha ishara ya bao 2 na anaefuata ni Opudo ambaye anaonyesha ishara ya Tano kwa timu tutakayo cheza nayo tenana mwisho ni Golikipa mahiri   Kikosi cha Timu ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Mara Kabla ya mechi Timu ya Waandishi wa Habari Mkoani Mara Ambayo ilianza kipindi cha Kwanza Katika uwanja wa Posta Musoma Ambapo Timu hiyo iliibuka na ushindi 2-1 Timu ya waandishi wa habari mkoani mara jana imeibuka na mshindi katika mchezo dhidi ya Timu ya mamlaka ya mapato Tanzania mkoani hapa kwa jumla ya mambo 2-1 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Posta manspaa ya musoma. Timu ya Mamlaka ya mapato ndio walikua wa kwanza kuliona lan

AMSHITAKI MKEWE BAADA YA KUZAA MTOTO MWENYE SURA MBAYA, ASHINDA KESI ALIPWA MAMILIONI YA PESA

Image
Hii ndo Picha ya Mwanamke huyo anaonekana kabla na baada ya kufanyiwa Oparesheni Mwanaume mmoja nchini China alishtuka baada ya mkewe kuzaa mtoto mwenye sura mbaya na aliamua kumfikisha mkewe mahakamani kwa kutomjulisha kuwa sura yake nzuri ilitokana na operesheni za kubadilisha sura, alishinda kesi na kuzawadia fidia ya mamilioni. Wakati Jian Feng alipomuona mtoto wake mchanga kwa mara ya kwanza alishtuka sana. Mtoto wake huyo wa kike alikuwa na sura mbaya kiasi cha kwamba alishindwa kuamini kuwa mkewe aliyekuwa akionekana mrembo sana angeweza kuzaa mtoto kama huyo. Jian alimgeuzia kibao mkewe na kumshtumu kuwa aliisaliti ndoa yao na kufanya mapenzi nje ya ndoa yaliyopelekea kuzaliwa kwa mtoto huyo. Baada ya hali kuwa tata, mkewe alilazimika kutoboa siri kuwa urembo wa sura yake unatokana na operesheni zilizomgharimu zaidi ya dola 100,000 ili kuirekebisha sura yake aonekane mrembo. Mkewe alisisitiza kuwa mtoto huyo ni wa kwao. Jian alikasirika sana kusikia hivyo

JOHN MNYIKA ATOA WITO KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KUTOA RASIMU YA SERA YA GESI ASILIA KWA LUGHA YA KIINGEREZA NA KISWAHILI

Image
Mbuge wa Ubungo John Mnyika Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), amepingana na hatua ya Wizara ya Nishati na Madini kutoa rasimu ya sera ya gesi asilia kwa Lugha ya Kiingereza pekee na kutoa wito sera hiyo kuandikwa pia katika lugha ya Kiswahili. Mnyika alisema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari jana na kumtaka Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo, kuutangazia umma kwamba, rasimu hiyo itatolewa pia kwa lugha ya Kiswahili na kwamba, ichapwe katika vyombo vingine vya habari. “Izingatiwe kuwa napinga hatua ya Wizara ya Nishati na Madini kuchapa rasimu ya Sera ya Taifa ya Gesi Asili kwa Lugha ya Kiingereza pekee kwenye baadhi ya magazeti tarehe 2 Novemba 2012, huku Katibu Mkuu wa Wizara hiyo akitoa mwito kwa wadau na Watanzania wote kutoa maoni hali, ambayo itakuwa ni kikwazo kwao kushiriki katika mchakato wa maandalizi ya sera yenye kuzingatia maslahi ya taifa,” alisema Mnyika katika taarifa hiyo. Alisema kitendo cha Bodi mpya ya Shirika l

MWANACHUO WA CHUO CHA MUSOMA UTALII ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA YA KUMCHOMA VISU MWANACHUO MWENZAKE KISA WIVU WA KIMAPENZI

Mwanachuo wa chuo cha musoma utalii cha mjini Musoma Rose Kanyambo (21),ameshambuliwa kwa kisu mgongoni na ubavuni na mwanachuo mwenzake John Ogolla kutokana na wivu wa mapenzi. Kwa mujibu wa Taarifa toka kwa mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Mara Irege Ngaregeza, amesema kuwa binti huyo alifikishwa hospitalini hapo siku ya ijumaa Novemba 2 mwaka huu, ambapo binti huyo alikuwa na jeraha la kuchomwa kisu mgongoni na ubavuni na alifikishwa hospitalini hapo akiwa na hali mbaya lakini madaktari walijitahidi kuokoa maisha yake na sasa anaendelea vizuri. Akizungumza na waandishi wa habari kwa taabu wodini binti huyo amesema kuwa siku ya ijumaa majira ya saa mbili asubuhi akiwa chuoni maeneo ya Kamunyonge manispaa ya musoma ,  Mwanachuo mwenzake anaefahamika kwa jina John Ogolla alitokea   chuoni hapo na kuanza kumshambulia kwa kumchoma kisu mgongoni mara mbili   na ubavuni ambpo hali hiyo ilimpelekea kutokwa na damu nyingi ambapo alifanikiwa kukimbia hadi alipokuwa anaishi si

MREMBO KUTOKA MARA ASHIKA NAFASI YA PILI KATIKA FAINALI ZA REDDS MISS TANZANIA 2012 HONGERA HOMELAND ENTERTAINMENTS

Image
Shindano la kumtafuta Mrembo wa Redds Miss Tanzania 2012 limemalizika siku ya Jumamosi huku mrembo Brigette Alfred kutoka Kitongoji cha Sinza, ameibuka mshindi katika shindano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Pearl Pub, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam. Mrembo huyo kutoka kituo cha Sinza na baadaye kuingia katika shindano la Kanda ya Kinondoni, kwa ushindi huo amejitwalia zawadi ya gari aina ya Noah na kitita cha sh milioni 8 zilizotolewa na mdhamini mkuu wa shindano hilo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original. Mshindi wa pili katika shindano hiloni Eugine Fabian kutoka Mara alijipatia sh milioni 6.2 akifuatiwa na Edda Sylvester kutoka Kitongoji cha Kigamboni, Kanda ya Temeke, aliyeondoka na sh milioni 4. Nafasi ya nne ilikwenda kwa Magdalena Roy aliyeondoka na sh milioni 3 na Happiness Daniel alishika nafasi ya tano na kujitwalia sh milioni 2.4. Walishika nafasi ya sita hadi 15, kila mmoja alijinyakulia sh milioni 1.2 na

KUACHWA KUACHWA KUACHWA NI SHUGULI PEVU

Image
Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza ambaye hakuridhishwa na uamuzi wa mpenzi wake kuachana naye, aliamua kumaliza hasira zake kwa kuzamisha meno yake kwenye uume wa mpenzi baada ya kujifanya anaomba msamaha ili uhusiano wao uendelee. Sinead Walker, mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa Bath, Somerset nchini Uingereza alienda kwa mpenzi wake kwaajili ya kuomba msamaha ili mapenzi yao yaendelee kama zamani. Lakini ghafla mwanamama huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja, alibadili uamuzi wake wa kuomba msamaha na kuamua kumshambulia mpenzi wake Vincent Rennoldson mwenye umri wa miaka 42 kwa kuyabinya kwa nguvu makende yake kabla ya kuamua kuzamisha meno yake ili aukate uume wake. Mahakama ambayo inasikiliza kesi ya mama huyo kujaribu kuzinyofoa hazina za mpenzi wake, iliambiwa kuwa Sinead akiwa amelewa alienda nyumbani kwa mpenzi wake akisema amekuja kuomba msamaha baada ya kumshambulia Vincent wiki mbili zilizopita baada ya Vincent kuamua kuvunja uhusiano wao. "Alinisukum

SIMU BANDIA UGANDA KUZIMWA 2013 TANZANIA, RWANDA NA BURUNDI PIA WAJADILI KUKAMILISHA ZOEZI HILO

Image
Uganda inachukua hatua Sawa na Kenya ambayo ilizima simu za watu zaidi ya Milioni Moja Uganda imeamua kusitisha mipango yake ya kuzima simu ghushi hadi tarehe moja mwezi Julai mwaka 2013. Hatua ya serikali inayolenga kuzuia simu bandia kutumika katika mitandao ya simu nchini humo ilikuwa imepangiwa kuafikiwa mwishoni mwa mwezi huu.   Kenya iliweza kuchukua hatua sawia na hii mwezi Oktoba na kuzima simu za zaidi ya watu milioni moja. Tume ya mawasiliano ya Uganda, imependekeza kuwa takriban asilimia kumi na tatu ya simu milioni kumi na saba za rununu Afrika Mashariki ni ghushi. Watumiaji wa simu hizo, wana hadi mwezi Machi kuhakikisha kuwa kadi zao zimesajiliwa na tume hiyo. Pia wametakiwa kubaini nambari yao ya kutambua simu ijulikanayo kama IMEI (International Mobile Equipment Identity) na ambayo huwa ipo kwenye simu halali. Simu ghushi kawaida huwa hazina nambari hii ya utambulisho.